Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa .amekutana na Mkurugenzi Mtendaji wa JOC Bw. Qin
Mengwei (Kulia). na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Namera Group of
Industries Bw. Hamza Rafiq Pardesi (kushoto mwenye miwani nyeusi) .
Wakurugenzi hao wameahidi kununua pamba yote itakayozalishwa.Nchini
Tanzania.Waziri Mkuu amekutana na viongozi hao leo, Februari 12, 2018
Ofisini kwake jijini Dar es Salaam
WAZIRI
MKUU. Kassim Majaliwa. amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa
viwanda vikubwa viwili vya kuchakata pamba cha Namera Group of
Industries,na JOC. Wakurugenzi hao wameahidi kununua pamba yote
itakayozalishwa nchini kuanzia msimu huu.Waziri Mkuu amekutana na
viongozi hao leo, Februari 12, 2018 Ofisini kwake jijini Dar es
Salaam.PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa
viwanda vikubwa viwili vya kuchakata pamba ambao wameahidi kununua pamba
yote itakayozalishwa nchini kuanzia msimu huu.Viongozi hao ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Namera Group of Industries Bw. Hamza
Rafiq Pardesi na Mkurugenzi Mtendaji wa JOC Bw. Qin Mengwei ambao kwa
pamoja wameahidi kununua pamba yote itakayozalishwa.
Waziri
Mkuu amekutana na viongozi hao leo (Jumatatu, Februari 12, 2018) jijini
Dar es Salaam na amesema kwamba wakulima waliitikia wito wa Serikali wa
kufufua zao hilo, hivyo mwaka huu wanatarajia kupata mavuno
mengi.Waziri Mkuu amewataka viongozi hao wajiandae kununua pamba nyingi
kwa sababau mwaka huu wakulima wamelima pamba ya kutosha baada ya
Serikali kuwahamasiha waongeze uzalishaji kwa kuwa kuna soko la uhakika.
Amesema
hatua hiyo imekuja baada ya Rais Dkt. John Magufuli kutoa maelekezo ya
uhamasishaji wa kilimo hasa mazao makuu ya biashara, tayari tija imeanza
kuonekana ambapo zao la korosho limepata mafanikio makubwa na sasa
linafuatia zao la pamba.
Waziri
Mkuu amesema Serikali inashiriki kikamilifu katika usimamizi wa zao la
pamba kuanzia hatua za maandalizi ya shamba kwa wakulima kuelekezwa
kulima kitaalam, upatikanaji wa pembejeo hadi masoko, hivyo amewaalika
viongozi hao kushiriki katika mkutano utakaowakutanisha wafanyabiashara
wote wa zao hilo.
“Mimi
mwenyewe mwezi huu nitakuwa na ziara ya kikazi mkoani Mwanza, kwa hiyo
tarehe 21, Februari, nimeitisha mkutano wa wafanyabiashara wote wa pamba
nchini iwe ni wanaosokota nyuzi, kuchambua pamba au kukamua mbegu za
pamba, ili mradi wanajihusisha na pamba nanyi naomba muwepo”.
Waziri
Mkuu amesema Serikali imefurahishwa na uamuzi wao wa kutaka kununua
pamba yote itakayozalishwa nchini kuanzia msimu huu kwani ni faraja kwa
Taifa kwa sababu wakulima walipunguza uzalishaji baada ya kukosa soko la
uhakika.Kwa upande wao, Bw. Pardesi na Bw. Qin wamemuhakikishia Waziri
Mkuu kwamba kampuni zao zinauwezo wa kununua pamba yote inayozalishwa
nchini na kuichakata katika viwanda vyao na kutengeneza nyuzi na nguo
zitakazouzwa nchini kwa bei nafuu.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATATU, FEBRUARI 12, 2018.
No comments:
Post a Comment