KUMUINUA MGENI RASMI MKUU WA WILAYA YA NJOMBE BI. SARAH DUMBA.
MKUU WA CHUO CHA VETA MONICA MBELE AKITOA UFAFANUZI NA MALENGO YA KUWAPATIA MAFUNZO KWA MADEREVA KWA KUWAFUATA HUKOHUKO WALIKO WALENGWA.
MKUU WA WILAYA YA NJOMBE BI.SARAH DUMBA AKITOA HOTUBA KWA WAHITIMU WA MAFUNZO YA UDEREVA WA GARI NA PIKIPIKI KWA TARAAFA YA IGOMINYI.
MJASILIA MALI TOKA VETA SONGEA MSHONAJI WA NGUO AINA YA BATIC BI.LUCY AKIONESHA SAMBO.
MRATIBU WA MAFUNZO YA MUDA MFUPI VETA SONGEA KWA MKOA WA RUVUMA NA NJOMBE SILVESTER NDALLAH AKITOA MAELEKEZO JUU YA UTARATIBU WA KUCHUKUA VYETI KWA WAHITIMU.
WAHITIMU WA MAFUNZO YA UDEREVA WAKIWA NDANI YA SALE.
AFISA TARAAFA YA IGOMINYI ELLY NGOLE AKIAHIRISHA SHEREHE ZA WAHITIMU WA MAFUNZO YA UDEREVA WA MAGARI NA PIKIPIKI LUPONDE.
MKUU WA WILAYA YA NJOMBE SARAH DUMBA AKIWA NA MKURUGENZI WA CHUO CHA VETA MONICA MBELE WAKITOKA NJE TAYARI KWA SAFARI.
Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi. Sarah Dumba Jana Amefunga Mafunzo ya Madereva wa Magari na Pikipiki wa Kata Saba za Tarafa ya Igominyi Pamoja na Kuwatunukia Vyeti Wahitimu 297 wa Mafunzo Hayo.
Akiongea Wakati wa Kufunga Mafunzo Hayo Bi.Dumba Amewataka Madereva Hao Kuutumia Ujuzi Walioupata Katika Mafunzo Hayo Ili Kuepusha Ajili Zisizo za Lazima Zinazoonekana Kuongezeka Kutokana na Madereva Wengi Kutokuwa na Ujuzi wa Vyombo Wanavyoendesha.
Wakiongea Wakati wa Kufungwa Kwa Mafunzo Hayo Baadhi ya Viongozi wa Veta Akiwemo Mkuu wa Chuo cha Veta Songea Bwana Gidion Olelairumbe na Mkurugenzi wa Veta Kanda ya Nyanda za Juu Bi. Monica Mbele Wamewaomba Maderevaa Hao Kuwa Mabalozi wa Madereva Ambao Hajapatiwa Mafunzo na Kuwataka Kuwahamasisha Madereva Ambao Hawajapatiwa Mafunzo Kujiandiksha Ili Wapatiwe Mafunzo.
Maro Chacha ni Afisa Usalama Barabarani Mkoa wa Njombe Ambaye Amewataka Madereva Hao Kuendesha Vyombo Vyao Kwa Kufuata na Kuzingatia Sheria za Barabarani Pamoja na Kutii Sheria Bila Shuruti
Kwa Upande Wao Wahitimu wa Mafunzo Hayo Wamesema Wamenufaika na Mafunzo Hao na Kueleza Kuwa Yamewasaidia Kufahamu Sheria za Barabari na Pia Zitasaidia Kupunguza Ajali Zisizo za Lazima.
Mafunzo Hayo ya Wiki Mbili Yaliyoanza Mwezi Disemba 31 Mwaka Jana Hadi Januari 24 Mwaka Huu Kwa Awamu Tofauti Ambapo Wahitimu Mia Mbili Tisini na Saba Wamehitimu Mafunzo Hayo.
Mafunzo Hayo Yanatarajiwa Kuendelea kuhitimishwa Kesho Katika Kijiji cha Igima Wilayani Wanging'ombe na Kata Nyingine Zikiwemo Lugenge na Ninga na maeneo mengine yaliyokwisha kupata mafunzo hayo.
No comments:
Post a Comment