WANANCHI WAKIELEKEA HOSPITALI YA KIBENA KWA MAANDAMANO HUKU WAKIIMBA NYIMBO
MSURURU WA MAGARI BAADA YA KUONA WANANCHI WAKO MBELE NA BARABARA IMETAWALIWA NA WAO WENYEWE
HAPA WAPO KITUO CHA DARADARA KIBENA HOSPITALI
HAPA NI HOSPITALI YA KIBENA AMBAPO WANANCHI WAMEFIKA NA KUINGIA KWENYE WODI YA WANAUME NA KUMUANGALIA MAJERUHI ALIYEDAIWA KUPIGWA RISASI
HUYU NDIYE MAREHEMU Basilius Ngore Ambaye Amedaiwa Kufariki Kwa Kupigwa Risasi Na Watu Wanaodaiwa Kuwa Ni Askali Wa Polisi Enzi Za Uhai Wake Alikuwa Fundi Ujenzi
HALI iLIKUWA HIVI KWENYE KITUO CHA DARADARA KIBENA KARIBU NA HOSPITALI YA KIBENA WANANCHI WAMEKUSANYIKA WAKIWA HAWAELEWI KINACHOENDELEA HUKU WENGINE WAKIWASHA MOTO BARABARANI KWENYE MOSHI UNAOONEKANA HUO.
KIKOSI CHA ASKALI WA POLISI WAKIWA KWENYE MARI YAO HUKU WANANCHI WAKIWATAZAMA KWA HASIRA KWA KUWA NDUGU ZAO MMOJA KAPOTEZA MAISHA NA MMOJA KARAZWA HOSPITALI KWA KUJERUHIWA.
JAZBA ZA WANANCHI ZA SABABISHA KUWASHA MOTO BARABARANI KWA KUFUNGA BARABARA
HAPA NI ENEO LA MTO RUHUJI NJIAPANDA YA BARABARA YA MAKETE ,MAKAMBAKO NA NJOMBE WANANCHI PIA WAFUNGA BARABARA KWA MAWE NA KULILAZIMU JESHI LA POLISI KUTUMIA NGUVU KUBWA YA KULIPUA MABOMU KUWATAWANYA.
BIASHARA NYINGINE ZILIKUWA ZIKIENDELEA MAENEO YA KITUO KIKUU CHA MABASI NJOMBE MJINI LAKINI HALI YA TAHARUKI IKAANZA BAADA YA KUANZA KUFUNGWA BARABARA YA NJOMBE SONGEA ENEO LA STENDI YA NJOMBE MJINI
HUYU NI MAJERUHI FRED SANGA AMBAYE AMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA KIBENA KWA MATIBABU ZAIDI BAADA YA KUDAIWA KUPIGWA NA RISASI
HAPA NI KIBENA WENGINE WAMEKAA KATIKATI YA BARABARA YA LAMI HAKUNA MAGARI KUPITA
HUU NI MSURURU WA MAGARI WAKATI WA MAANDAMANO YA WANANCHI HAO
WAANDISHI WA HABARI WATATU WANAOONEKANA MBELE YAKO HUKU WALIKO MBELE WANAOPANDISHA BARABARA YA KUSHOTO NI WANANCHI WANAELEKEA BARABARA YA KUELEKEA MAKETE WANAKIMBIA MABOMU YANAYORIPULIWA NA ASKALI WA POLISI.
Njombe.
Hali ya tahaluki jana ilitanda kwa wakazi wa Mji wa Njombe kufuatia kusikika
milio ya mabomu kila kona baada ya polisi wa doria juzi usiku kuua raia mmoja kwa
kumpiga risasi na kujeruhi mwingine katika klabu cha pombe cha Nyondo Mtaa wa
Kambarage.
Kitendo hicho kilisababisha wananchi kuandamana hadi
hospitali ya Mkoa wa Njombe Kibena anapotibiwa majeruhi huyo pamoja na kuhifdhiwa
mwili marehemu.
Wananchi hao walisema wanaandamana ili kupinga mauji ya
askari dhidi ya raia.
Aliyeuawa katika tukio hili ni Basil Ngole mkazi wa Mtaa wa
Kambarage na aliyejeruhiwa ni Fred Sanga mkazi wa mtaa huo ambapo kwa sasa
amelazwa katika hospitali hiyo.
Kufuatia tukio hilo wananchi walikusanyika hospitalini hapo
majira saa moja asubuhi kupinga polisi kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya
raia, huku wakipaza sauti za kulitaka jeshi la polisi kugharamia mazishi ya
marehemu pamoja na matibabu ya aliyejeruhiwa.
Kutokana na kadhia hiyo polisi walifika eneo la tukio na
kuanza kuwatawanya waandamanaji hao kwa mabomu ya machozi na kupelekea
mwananchi mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Mandele dereva wa bodaboda mjini
Njombe kujeruhiwa.
Kitendo hicho kiliamsha hasira kwa wananchi na kuanza vurugu
kuziba barabara na mawe na kuchoma mataili ya gari barabarani.
Wakizungumzi tukio hilo baadhi wa wananchi mjini hapa,
walilaani kitendo cha polisi kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya raia wasiokuwa
na hatia, huku wakiomba askari aliyetekeleza mauaji hayo na majeruhi
kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
Emanuel Filangali mkazi wa Njombe alisema hata kama marehemu
na majeruhi na raia wengine walikuwa na kosa la kunywa pombe nje ya muda katika
klabu hicho walipaswa kukamatwa na siyo sakari kuwapiga risasi na kusababisha kifo
pamoja na majeruhi.
“Imekuwa kawaida kwa polisi kutumia nguvu kubwa dhidi ya
raia, kama wao ndio wanashiriki kuua raia badala ya kuwalinda na mali zao kama
ilivyosheria za jeshi la polisi, sasa wanafanya kazi gani,” alisema Emmanuel
Ngalime.
Robert Shemajabu mkazi wa Njombe, alilitaka jeshi la polisi
kuchukua jukumu la kumzika marehemu na kuwatibu majeruhi wa vurugu hizo na
kuiomba serikali kumchukulia hatua kali askari aliyehusika na tukio hilo.
“Wananchi tumechoka dhuluma dhidi ya polisi walahi tunataka
amani, lakini vitendo vy polisi kuendelea kuua raia havikubaliki hata kidogo,
ni lazima jeshi la polisi litende haki kwa kuuzika mwili wa marehemu na
kuwatibu waliojeruhiwa katika tukio hili, pili tunaomba askari aliyeua sheria
ichukue mkondo wake maana hakuna mtu aliye juu sheria,” alisema Shemabu na
kuongeza.
“Kama huyu askari hakutumwa kutenda haya aliyoyatenda na
imani haki itatendeka, hatutaki kuona wakipindisha sheria mpaka sasa hivi
hawataki kumtaja askari aliyeua,” alisema.
Diwani wa Kata ya Njombe Mjini Agrey Mtambo alifika eneo la
tukio na kuwaomba wananchi kudai haki yao lakini pia akiwataka kulinda usalama
wao.
“Katika mazingira kila mmoja wetu aidai haki hii lakini pia
akilinda usalama wake, tunachotaka hawa askari walioua nao wawajibishwe kwa
mujibu wa sheria za nchi hii,” alisema Mtambo na kuongeza.
“Tungeweza kuchanga
kwa ajili ya mazishi na kumhamisha mgongwa lakini hatuwezi kufanya hivyo maana
hili jukumu ni polisi waliotekeleza haya na RPC (Kamanda wa Polisi Mkoa)
tumeshamueleza,” alisema.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Franco Kibona alipofuatwa
na waandishi wa habari kutolea ufafanuzi suala hilo alisema kwa kifupi; “siwezi
kuzungumzia suala hili kwa sasa wakati hali haijatulia”.
Hata hivyo alifika eneo la tukio na kuwasihi wananchi
kutulia kwani madai yao yanashughulikiwa.
Hadi Mwandishi wa gazeti hili anatoka eneo la tukio majira
ya saa tisa alasiri Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa ilikuwa inaeendelea na
kikao cha kujadili hali hiyo, huku hali ya usalama ikiwa haijatulia kwani
mabomu ya machozi yalikuwa yakiendelea kusikika kuwatawanya waandamanaji
waliokuwa na chupa za maji kukabiliana na mabomu ya machozi.
Hali hiyo tahaluki ilisababisha maduka mjini Njombe
kufungwa, wafanyabiashara wakihofia hali ya usalama, huku waandamanaji wakiziba
barabara kwa mawe kuzuia magari na
kuchoma mataili barabarani hali iliyopelekea magari ya polisi kuzunguka kila
kona huku wakirusha mabomu ya machozi kuwatawanya waandamanaji.
Kwa Upande wake Majeruhi wa tukio hilo Fred Sanga
akizungumza kwa taabu katika Hospitali ya Kibena anakopatiwa aliliambia gazeti
hili kuwa, wakati akiwa katika klabu hicho askari polisi wa doria ambao hawakujalia sare
za jeshi waliingia klabuni hapo na kuwaamuru yeye pamoja na wateja wengine
wakae chini hali iliyozua mzozo.
Alisema kufuatia hali hiyo polisi walilazimika kufyatua
risasi ambazo zilimpata yeye na marehemu, ambapo yeye alijeruhiwa sehemu za
siri na makalio.
Katika eneo la polisi mwandishi wa gazeti hili
alishuhudia baadhi ya raia wakishushwa kwenye gari la polisi kutokana na vurugu
hizo na kuwekwa ndani. Huku kukiwa taarifa za kuvunjwa kwa nyumba ya askari
mmoja anayedaiwa kutekeleza tukio hilo ambaye hakuweza kufahamika, ingawa wakazi
wa Mtaa wa Kambarage walikuwa wakimtaja kwa jina la Jack.
........END.
No comments:
Post a Comment