MTOTO ALIYETUPWA NA MAMA YAKE AMBAE ALIKUWA MUUZAJI WA POMBE ZA KISASA KWENYE BAR MOJA ILIYOPO JIRANI NA NYUMBANI KWAKE MTAA WA NATIONAL HOUSING MJINI NJOMBE
MASHUHUDA WA TUKIO WAKIWA PAMOJA NA ASKALI WA POLISI MKOA WA NJOMBE
MWENYEKITI WA MTAA WA NATIONALHOUSING MJINI NJOMBE BWANA MAKWETA AKIZUNGUMZA BAADA YA KUOKOTWA MWILI WA MTOTO MCHANGA HUYO.
Watu Watatu Wamefariki Katika Matukio Matatu Tofauti Mkoani Njombe Likiwemo la Mtoto Mchanga Aliyeokotwa Akiwa amekufa Eneo la Nationalhousing Mjini Njombe Huku Wengine Tisa Wakiwa wamejeruhiwa na Kulazwa Katika Hospitali Mbalimbali za Mkoa wa Njombe Baada ya Gari Walilokuwa Wakisafiria Kupata Ajali.
Kaima Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe Focus Malengo Amesema Katika Tukio la Kwanza Juni 22 Mwaka Huu Ambapo Mwanamke Mmoja Alijifungua Mtoto wa Kike na Kumtupa Nje ya Nyumba Anayoishi na Kwamba Jeshi Hilo Linamshikilia Kwa Mahojiano.
Kamanda Malengo Amesema Watu Wawili Wamefarika Kutokana na Ajili za Barabara Ikiwemo Ajali ya Gari Lenye Namba za Usajili T 965 BDM Aina ya Noah Walilokuwa Wakisafiria Kuacha Njia na Kupinduka na Kusababisha Kifo cha Ambwene Mgaya na Kusababisha Majeruhi Tisa.
Amesema Ajali Hiyo Imetokea Juni 22 Majira Saa Moja na Nusu Usiku Katika Kijiji cha Iboma Barabara Kuu ya Njombe na Kwamba Gari Hilo Lilikuwa Likiendeshwa na Nesfoli Kayombo.
Aidha Kamanda Malengo Amesema Ajali Nyingine Imetokea Juni 22 Saa Moja Usiku Eneo la Shule ya Viziwi Mjini Njombe Ambapo Adam Mng'ong'o Akiwa Anaendesha Pikipiki Yenye Namba za Usajili T 532 BYT Amefariki Papo Hapo Baada ya Kugongwa na Gari
Kaimu Kamanda Huyo wa Polisi Amesema Jeshi la Polisi Bado Linaendelea na Uchunguzi wa Matukio Hayo Huku Akiwataka Madereva Kufuata Sheria za Barabara na Kujali Watu Wengine Wanaotumia Barabara Hizo.
Wakati Huo Huo Jeshi Hilo Linamshikilia Mkazi wa Kijiji cha Mtila Sikujuwa Msemwa Kwa Tuhuma za Kumbaka Mtoto Wakike Mwenye Umri wa Miaka Mitatu na Kumsababishia Maumivu Makali.
Kaimu Kamanda Malengo Amesema Tukio Hilo Limetokea Juni 22 Majira ya Saa Sita Mchana Kijijini Humo na Kwamba Mtoto Huyo Amelazwa Kwa Ajili ya Matibabu.
No comments:
Post a Comment