CHANZO MBEYA YETU BLOG
Kaimu
Mwenyekiti wa TEKUASA Amani Simbeye akifungua mkutano kati ya waandishi
wa Habari na Waahadhiri wa Chuo kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU)
Waahadhiri wa Chuo kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU) wakifuatilia kwa umakini kikao hicho wakati kikiendelea
Kaimu Mwenyekiti wa TEKUASA Amani Simbeye pamoja na katibu wake wakisikiliza kwa umakini wahadhiri wakichangia hoja
Mmoja wa Waahadhiri wa Chuo kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU) , akikazia jambo ya yale ambayo yalikuwa yamezungumzwa
Mmoja
wa Waahadhiri wa Chuo kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU), akitila mkazo
na kujibu swali ambalo liliulizwa na mmoja wa waandishi wa Habari.
Waahadhiri wa Chuo kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU) wakipiga piga Meza kuashiria kuunga MKONO Hoja ilizo somwa.
Kikao kikiwa kinafungwa kwa Sala
Waahadhiri wa Chuo kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU) wakiwa wanaimba wimbo wa Solidarity
Kaimu
Makamu Mkuu wa Chuo Dr. Daniel Mosses Akiwa anauficha Uso akihofia
kupigwa picha na kuhojiwa na waandishi wa Habari kuhusiana na Mgogoro
unao endelea Chuoni hapo
HALI si Shwari Ndani ya Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji
(TEKU) baada ya Uongozi wa Chama cha Wahadhili wa Chuo hicho (TEKUASA) na
wanachama wake kutangaza mgomo wa kutotunga mitihani ya kufungia Mhula,
Mitihani ambayo inatarajiwa kufanyika Julai Mosi Mwaka huu kwa kile walichodai
Menejimenti ya Chuo kutotoa majibu ya matatizo yao.
Mgomo huo umetangazwa leo na Kaimu Mwenyekiti wa
Tekuasa Amani Simbeye katika Mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika
ukumbi wa Chuo hicho kilichopo Block T
kata ya Iyela Jiji na Mkoa wa Mbeya na kuhudhuriwa na zaidi ya Wahadhili 30.
Simbeye amesema kuna mambo
mengi na changamoto za elimu inayotolewa Chuoni hapo ambazo Menejimenti ya Chuo
inahusika moja kwa moja hivyo kuhatarisha mustakabali wa Elimu Nchini hususani
inayotolewa Chuoni hapo ambapo ameongeza kuwa zaidi ya yote ni kukosa ushirikishwaji
wa maamuzi yanayohusu Taaluma.
Kwa taarifa zaidi na madai ya
Wahadhili hao hadi kupelekea kususia kutunga mitihani ya kumaliza muhula
inatarajiwa kufanyika Julai Mosi Mwaka huu yameandikwa kwenye barua hapo chini lakini habari kamili
itawajia baadaye kwa Lugha ya Kiswahili endelea kuwa nasi.
No comments:
Post a Comment