picha ya zamani ya marehemu Chota.
MAREHEMU Mexon Chota katika picha yake aliyopiga siku za karibuni kabla hajazama kwenye bwawa la kampuni ya Tanwat akiwa na mama yake.
JITIHADA ZA WANANCHI WAKATI ZILIPOKUWA ZINAFANYIKA ZA KUUTAFUTA MWILI WA MAREHEMU MEXON CHOTA.
HATIMAE MWILI WA MAREHEMU WAPATIKANA SASA WANAUTOA MBELE YA BOAT NI MTAALAM TOKA WILAYANI MUFINDI AKIWA AMESHIKIRIA NGUO YA MAREHEMU TAYARI KWA KUTOKA NAO NJE YA MAJI.
TAYARI WAMEFANIKIWA KUUTOA KWENYE MAJI NA HAPA WANAULAZA KWENYE KARATASI ILI MAJI YAPUNGUE MWILINI MWAKE MAREHEMU MEXON CHOTA.
TAYARI WAMEKWISHA UFUNIKA MWILI WA MAREHEMU USIWAKIWE NA JUA NA KUGUSWA NA WADUDU KAMA NZI KWA KUWA ULIANZA KUHARIBIKA.
AFISA UPELELEZI WA JESHI LA POLISI WILAYA YA NJOMBE PHELISIAN KAMGISHA AKIWA AMEONGOZANA NA DR WA KIBENA WAKIWASILI ENEO LA TUKIO KUUPIMA MWILI WA MAREHEMU NA KUUOSHA TAYARI KWA MAZISHI.
AFISA TARAAFA WA NJOMBE MJINI LILIANI NYEMELE KWA MASIKITIKO MAKUBWA ANASOGEA KWENYEN MWILI WA MAREHEMU .
MWILI WA MAREHEMU TAYARI UMEKWISHA OSHWA NA TAYARI KWA KUAGWA.
WANANCHI NA NDUGU WANAUAGA MWILI WA MAREHEMU KATIKA BWAWA HILO ALIKOOKOLEWA.
AFISA TARAAFA WA NJOMBE MJINI AKIZUNGUMZA NA WANANCHI BAADA YA MWILI KUANDALIWA KWENDA KWENYE MAZISHI.
HAWA WATATU NI WATAALAM WA KUZAMA NDANI YA MAJI TOKA DAR MWENYE SUTI NYEUSI NI JOSEPH MAPUNDA ALIEONGOZA MSAFARA HUO NA WAWILI WATUMISHI WENZAKE.
KOTI NA VIATU KWAAJILI YA KUZUIYA BARIDI UKIWA NDANI YA MAJI NA VIATU KUZUIYA MIGUU ISIHARIBIKE UKIWA NDANI YA MAJI AMBAPO MTUNGI HUU UNA KILOGRAM 15 UNABEBWA NA KUZAMA NAO NDANI YA MAJI UKIWA UMEJAZWA HEWA SAFI YA KUVUTA MWANADAMU SAWA NA AKIWA NJE YA MAJI.
MTUNGI WA GESI KWAAJILI YA PUMZI WAKATI AKIZAMA NDANI YA MAJI NA UTUMIAPO HEWA YA MTUNGI HUU UNAUWEZO WA KUKAA ZAIDI YA SAA MOJA UKIWA KWENYE MAJI
BAADA YA KUWASILI WATAALAM TOKA DAR ES SALAAM DIVE INSTRUCTOR SEA BREASE MARINE JOSEPH MAPUNDA NA WENZAKE WAWILI WAKAANZA KUTOA ELIMU KWA UCHACHE BAADA YA WANANCHI KUTAKA KUFAHAMU MATUMIZI YA VIFAA WALIVYOKUJA NAVYO KUOKOLEA MWILI WA MAREHEMU.
MCHUNGAJI WA KANISA LA KILUTHEL TANZANIA USHARIKA WA KIBENA K.K.K.T NELSON KADUMA ALIONGOZA IBADA YA MAZISHI NA HAPA ANAWEKA MSALABA KWENYE KABURI LA MAREHEMU.
MAMA YAKE MAREHEMU MEXON CHOTA BI.LAINES MLIMBILA AKIWEKA TAJI KWENYE KABURI LA MTOTO WAKE ALIYEKUFA MAJI.Picha na Michael Ngilangwa.
Mazishi ya Mkazi Mmoja wa Kibena Mjini Njombe Mexon Nyekelela Chota Yamefanyika Leo Katika Makaburi ya Kibena,Ikiwa ni Baada ya Kupatikana Kwa Mwili wa Marehemu Uliokuwa Amezama Kwa Siku ya Tano Katika Mabwawa ya Kampuni ya TANWAT Mjini Njombe.
Mwili wa Marehemu Ulipatikana Leo Majira ya Saa Nane Mchana Ikiwa ni Baada ya Jitihada za Muda Mrefu za Wananchi na Viongozi Kuweza Kuutafuta Mwili Huo Bila Mafanikio Kutokana na Ukosefu wa Vifaa Vya Uokozi.
Akizungumza Mara Baada ya Kupatikana Kwa Mwili Huo Afisa Tarafa ya Njombe Mjini Bi Lilian Nyemele Ameishukuru Kampuni ya TANWAT Kwa Namna Ilivyoshiriki Katika Kusaidia Zoezi Hilo Pamoja na Wananchi Wote Walioshiriki.
Akizungumza Mara Baada ya Kuwasili Mkoani Njombe Mtaalam wa Uzamiaji Kutoka Jijini Dar Joseph Mapunda Anasema Kuna Haja Kwa Serikali ya Mkoa wa Njombe Kuanza Kutoa Mafunzo Kwa Wananchi na Wataalam Mbalimbali Ili Kuweza Kupata Wataalam wa Uzamiaji.
Aidha bwana Mapunda amesema fursa za kupata mafunzo ya kuogelea na uzamiaji ndani ya maji zinapatikana Dar es salaam ambapo taasisi na serikali zinatakiwa kuwaita wataalamu hao kufika mahala walipo wananchi na vijana na kupatiwa mafunzo hayo ili kuwapata vijana wenye utaaramu huo ikiwemo wananchi wenyewe kuwapeleka vijana wao kwenye vyuo hivyo ili kupata mafunzo hayo.
Kwa upande wao viongozi wa mitaa ya Kibena Pasval Kaduma na Faustini Mwenda wamesema kufuatia kutokea kwa tukio hilo la kuzama kwa kijana hiyo kampuni ya Tanwat kwa kushirikiana na viongozi wa serikali wasema haruhusiwi mtu yeyote kwenda kuvua samaki wala kuogelea katika mabwawa hayo kinyume na hapo hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.
Marehemu Mexon Nyekelela Chota Alizama Kwenye Mabwawa Hayo Mnamo March Mosi Mwaka Huu Majira ya Saa Kumi na Moja Jioni Wakati Akiwa na Wenzake Mara Baada ya Kumaliza Shughuli Zao za Sanaa na amepatikana jumanne march 5 na kuzikwa katika makaburi ya eneo la kanisa la romani la zamani mtaa wa kibena kati mjini Njombe.
No comments:
Post a Comment