WANAKWAYA KUTOKA MAKANISA MBALIMBALI YA MJINI NJOMBE WAPO KANISA LA MOROVIANI MJINI NJOMBE.
MWENYEKITI WA UMOJA WA AKINA MAMA WA KIKRISTO MJINI NJOMBE BI.GROLIA MLELE.
AFISA TAARAFA WA NJOMBE MJINI BI.LILIANI NYEMELE AKIMKARIBISHA MKUU WA MKOA ALIYEKUWA MGENI RASMI SIKU YA MAOMBI YA UMOJA WA AKINA MAMA WA KIKRISTO.
MKUU WA MKOA WA NJOMBE CAPTAIN ASERI MSANGI AKITOA HOTUBA KATIKA KANISA LA MOROVIANI MJINI NJOMBE.
wakina mama hapa wanatoka kanisani siku ya maombi katika kanisa la Moroviani mjini Njombe.
KWAYA ZA BURUDISHA KANISANI MARA BAADA YA HOTUBA YA MGENI RASMI.
MKUU WA MKOA WA NJOMBE AKEMEA PIA HALI HII YA UCHAFU MJINI NJOMBE NA KUWATAKA VIONGOZI KUSIMAMIA USAFII.
Serikali Mkoani Njombe Imesema Itawakamata na Kuwafunga
Wazazi Wote Walioshindwa Kuwapeleka Watoto Wao Shuleni Licha ya Kuchaguliwa
Kujiunga na Kidato Cha Kwanza Mwaka Huu.
Katika Agizi Hilo Serikali Imesema Hadi Kufikia March Kumi
Mwaka Huu Mzazi Yoyote Atakaesababisha Mtoto Wake Kushindwa Kuanza Shule
Atakamatwa na Kuwekwa Ndani Pamoja na Kuhojiwa Juu ya Sababu Mtoto Wake
Kushindwa Kuanza Shule.
Akizungumza na Umoja wa Wakina Mama wa Kikristo Mkoani
Njombe Mkuu wa Mkoa wa Njombe Kapteni Mstaafu Assery Msangi Amesema ni Aibu Kwa
Eneo la Njombe Mjini Kuona Hadi Sasa Kuna Wanafunzi Hawajaanza Shule na Hivyo
Kumuagiza Afisa Tarafa Kufuatilia Suala Hilo.
Katika Hatua Nyingine Mkuu Huyo wa Mkoa Amesikitishwa na
Kitendo Cha Kukithiri Kwa Uchafu Katika Baadhi ya Maeneo ya Mjini Njombe na
Hivyo Kuwataka Wananchi Kuzingatia Usafi wa Mazingira.
Kwa Upande Wake Mwenyekiti wa Umoja wa Wakina Mama Wakristo
Mkoani Njombe Bi Groria Mlele Amewashukuru Wakina Mama Wote Waliojitokeza na
Kufanikisha Maombi Hayo.
Umoja wa Wakina Mama Wakristo Mkoani Njombe Kwa Sasa Una
Jumla ya Makanisa Matano Yaliopo Mjini Njombe ambapo kwa mwaka huu maombi
yamefanyikia katika kanisa la Morovian mjini Njombe.
No comments:
Post a Comment