Monday, July 1, 2013
MUHASHAMU ASKOFU WA JIMBO LA LINDI BRUNO NGONYANI AMEZINDUA KONGAMANO LA UTOTO MTAKATIFU LINALOFANYIKA JIMBO LA NJOMBE JANA..
WATOTO WA KIPAPA WAKIWA KWENYE KONGAMANO HILO HAPO JANA
MUHASHAMU ASKOFU WA JIMBO LA LINDI AMBAE ALIKUWA MGENI RASMI HAPO JANA NA KUZINDUA KONGAMANO HILO LA WATOTO
MAPADRE KUTOKA MKOA WA IRINGA
MAPADRE WA JOMBO LA NJOMBE
MUHASHAMU ASKOFU ALFRED MALUMA AKIWASIHI WATOTO KUZINGATIA MAFUNZO WATAKAYOPEWA NA KUTUNZA MAADILI YA KIDINI
MKURUGENZI WA VIJANA NA WATOTO JIMBO LA NJOMBE PADRE CLEMENT MGOHELE AKITOA NASAHA KWA WATOTO HAO
MAPADRE WA KUTOKA JIMBO LA NJOMBE
MUHASHAMU ASKOFU WA JIMBO LA NJOMBE ALFRED MALUMA AKIWA NA MUHASHAMU ASKOFU WA JIMBO LA LINDI BRUNO NGONYANI
BAADA YA KUMALIZIKA KWA UFUNGUZI WA KONGAMANO HILO MUHASHAMU ASKOFU NGONYANI AKAANZA KUWASALIMU WATOTO KWA KUWASHIKA MKONO KILA MMOJA.PICHA NA MICHAELNGINGWA
Mhashamu Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Lindi Bruno Ngonyani Leo Amezindua Kongamano la Siku Nne la Utoto Mtakatifu
Kwa Mikoa ya Kusini Ambapo amewataka Watoto Wanaoshiriki Kongamano Hilo Kuwa Mabalozi Katika Jamii Katika Kutenda Matendo ya Kumpendeza Mungu.
Akizungumza Wakati wa Kufungua Kongamano Hilo Askofu Ngonyani Ameseam Kongamano Hilo Litasaidia Kwa Kiasi Kikubwa Kuwajenga Watoto Hao Katika Imani ya Kidini na Maadili Mema Huku Akiwataka Watoto Hao Kuwa Wavumilivu Kwa Kipindi Chote cha Mafunzo Yatakayotolewa Kwenye Kongamano Hilo
Aidha Askofu Ngonyani Amewataka Viongozi wa Dini Wakiwemo Watawa na Mapadri Kutumia Kongamano Hilo Kuwafundisha Watoto Hao Elimu ya Dini Ukiwemo Utawa na Upadri Pamoja na Usomaji wa Biblia.
Askofu Ngonyani Amewapongeza Viongozi wa Kanisa Katoliki la Njombe Kwa Kuandaa Kongamano Hilo Linalowakutanisha Watoto Kutoka Mikoa ya Njombe , Lindi Mbeya , Iringa na Ruvuma Ambalo Limelenga Kuwapa Mafunzo Mbalimbali ya Kidini na Jamii Inayowazunguka .
Akielezea Lengo la Kongamano Hilo Padre Clement Mgohele Ambaye ni Mkurugenzi wa Vijana na Watoto wa Kanisa Katoliki Jimbo la Njombe Amesema ni Kutoa Semina Kwa Watoto Hao Juu ya Maadili Mema Katika Jamii na Mafundisho ya Maandiko Matakatifu Ikiwemo Kuyasoma na Kuyaelewa Maandiko Hayo.
Ameongeza Kuwa Kongamano Hilo Litasaidia kuwajenga watoto katika Maadili Kwa Vijana Hasa Katika Kizazi Hiki Ambacho Vijana Wengi Wamejiingiza Katika Tabia na Matendo Maovu Yanayoshusha Maadili ya Mtanzania.
Zaidi ya Watoto Elfu Mbili wa Kikristo wa Kanisa Katoliki Kutoka Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini Wanashiriki Katika Kongamano Hilo la Siku Nne Mjini Njombe.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment