Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Sunday, June 30, 2013

MAADHIMISHO YA SIKU YA SERIKALI ZA MITAA KUFANYIKA KITAIFA MOROGORO




Hon. Mayor Amir J. Nondo
Manispaa ya Morogoro imeteuliwa na kamati ya Utendaji ya ALAT Taifa mwaka huu wa 2013 kuwa mwenyeji wa maadhimisho ya Kitaifa ya sherehe ya siku ya Serikali za Mitaa Tanzania. Manispaa ya Morogoro kama mwenyeji wa maadhimisho hayo tunawaalika wananchi wote, wadau mbalimbali, na Taasisi zote za Mamlaka ya Serikali za Mitaa kushiriki kikamilifu wakati wa maadhimisho hayo.
   Sherehe hizi zitafanyika kwenye uwanja wa Jamhuri kuanzia tarehe 24/06/2013 na kufikia kilele chake tarehe 01/07/2013. Matukio Muhimu wakati wa maadhimisho haya yatakuwa ni pamoja na:-
     - Maonyesho mbalimbali ya kazi zinazofanywa na Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania
     - Ufunguzi na Uzinduzi wa Miradi mbalimbali ya Maendeleo
    - Semina na Makongamano mbalimbali juu ya uboreshaji wa huduma za Serikali za Mitaa
    - Matamasha na mashindano mbalimbali ya michezo na fani za sanaa.

MEYA  MH. AMIRI J. NONDO PAMOJA NA MKURUGENZI WA MANISPAA YA MOROGORO ANAWAKARIBISHA WANANCHI NA WAKAZI WOTE KUSHIRIKI KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA SERIKALI ZA MITAA TANZANIA

No comments:

Post a Comment