Mratibu Wa Mafunzo Ya Usalama Wa Barabarani Kutoka Future World V.T.C Yusto Walisimba Akizungumza Na Wahitimu Hao
ALAMA ZA BARABARANI WALIZOPEWA
WAHITIMU WANATUNUKIWA VYETI VYA KUHITIMU MAFUNZO HAYO
KAMANDA WA KIKOSI CHA USALAAMA BARABARANI MKOA WA NJOMBE KALVIN NDIMBO AKIWA KWENYE HAFRA HIYO FUPI YA KUWATUNUKU VYETI WAHITIMU WA MAFUNZO YA UDEREVA
MBWILO AKIPOKEA CHETI CHA MAFUNZO YA UDEREVA
WAHITIMU WA MAFUNZO YA UDEREVA WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA MGENI RASMI KAIMU KATIBU TAWALA MKOA LAMECK NOA PAMOJA NA WAKUFUNZI KUTOKA VTC DAR ES SALAAM PAMOJA NA JESHI LA POLISI KUPITIA KITENGO CHA USALAMA BARABARANI.
Mkuu Wa Mkoa Wa Njombe Dkt Rehema Nchimbi Amewataka Madereva Wa Vyombo Vya Moto Hususani Madereva Bodaboda Kujitokeza Kwa Wingi Kupatiwa Mafunzo Na Leseni Za Udereva Ili Waweze Kufuata Sheria Na Kanuni Za Barabarani Na Kupunguza Matukio Ya Ajali Ambazo Zimekuwa Zikijitokeza Mkoani Njombe Kwa Kukiuka Sheria Hizo.
Akizungumza Wakati Wa Kufunga Mafunzo Ya Udereva Kwa Wamiliki Na Madereva Wa Pikipiki 111 Kwa Niaba Ya Mkuu Wa Mkoa Wa Njombe Dkt Rehema Nchimbi,Kaimu Katibu Tawala Mkoa Wa Njombe Lameck Noa Amewataka Madereva Hao Kufuata Sheria Za Usalama Wa Barabarani Kwa Kuacha Kuendesha Vyombo Vya moto Kwa Mwendo Kasi Na Kuendesha Kwa Sifa.
Aidha Kaimu Katibu Tawala Huyo Noa Amesema Sheria Na Alama Mbalimbali Za Barabarani Madereva Hao Wameweza Kufundishwa Na Wakufunzi Wa Kutoka Chuo Cha V.T.C Cha Future World Insititute Cha Dar Es Salaam Ikiwemo Sheria Na Kanuni Za Uendeshaji,Alama Za Barabarani, Kupunguza Mwendo Kasi Maeneo Mhimu Na Kutopiga Honi Maeneo Ya Mahakama Na Hospitali.
Awali Akizungumza Mratibu Wa Mafunzo Ya Usalama Wa Barabarani Kutoka Future World V.T.C Yusto Walisimba Mkola Ametaka Jeshi La Polisi Kuhakikisha Linawakamata Baadhi Ya Madereva Wote Wanaoendesha Vyombo Vya Moto Huku Wakiwa Hawana Leseni Kwani Ajali Nyingi Hapa Nchini Zinasababishwa Na Madereva Wazembe Wasiyo Na Leseni.
Akisoma Risala Fupi Ya Washiriki Wa Mafunzo Ya Usalama Barabarani Na Polisi Jamii Kwa Niaba Ya Washiriki Wengine Jeniko Lusungu Mbwilo Amesema Jumla Ya Wahitimu 111 Wa Kutoka Maeneo Mbalimbali Ya Mkoa Wa Njombe Walihudhuria Mafunzo Hayo Lakini Ni Wahitimu 62 Waliotunukiwa Vyeti Vya Udereva Siku Ya Leo Kutokana Na Sababu Mbalimbali.
Mafunzo Hayo Yametolewa Na Jeshi La Polisi Mkoa Wa Njombe Kwa Kushirikiana Na Chuo Cha Future World Vocation Institute Kutoka Dar Es Salaam Kwa Kuelimisha Mambo Mbalimbali Wanayotakiwa Kuzingatia Madereva Wakiwa Kazini Kuwa Ni Pamoja Na Kuzingatia Usafi Na Ulinzi Shirikishi Kwa Kuwafichuwa Waharifu Mbalimbali Kwani Wao Ndiyo Wahusika Wa Kuwasafirisha Waharifu.
...............................................................................................................................................................................
NI VIZURI KUSHIRIKI MAFUNZO ILI KUONDOA UJINGA WA BARABARANI
ReplyDelete