Na Catherine Sungura, Mbeya
Waziri
wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Mhe. Ummy Mwalimu
amefanya ziara katika hospitali zilizopo Mbeya na kuzitaka hospitali
zinazotumia mfumo wa ukusanyaji mapato wa kieletroniki wasibweteke na
mapato wanayoyakusanya kila siku.Rai
hiyo imetolewa na aziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Mh. Ummy Mwalimu wakati alipotembelea hospitali ya rufaa ya
kanda ya mjini Mbeya.
Ummy
alisema ukusanyaji wa mapato kwa mfumo huu unasaidia kwa kiasi kikubwa
katika kuboresha huduma za afya nchini ikiwemo ununuzi wa dawa, vifaa na
vifaa tiba pamoja na utoaji wa motisha kwa watumishi."Bado
tunatambua hali ya uhaba wa upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kuanzia
ngazi zote, tukiweza kusimamia vizuri hili tutafanikiwa," alisema.
Aidha
alisema wanatarajia katika serikali ya awamu hii bajeti ya dawa
itaongezeka zaidi ya mara tatu kulinganisha na bajeti za nyuma, hivyo
wameishauri Bohari Kuu ya Dawa (MSD) wanunue dawa toka kwa wawekezaji wa
hapa nchini ambapo itakua na bei nafuu na itaongeza tija na upatikanaji
wa dawa kwa haraka.
Waziri Ummy Mwalimu aliutaka Mkoa kufuatilia, kuwafichua na kuwachukulia hatua wale wote watakaojihusisha na wizi wa dawa."Tunao
watumishi wachache wa afya ambao wanahujumu na kuiba dawa na kuzipeleka
kwenye maduka ya dawa binafsi, hao hatutowafumbia macho na kuwapeleka
mahakamani"
Kuhusu
upungufu wa watumishi wa kada ya afya nchini, Waziri wa afya alisema,
nchi ina upungufu wa asilimia 52, hivyo serikali inatarajia kuajiri
watumishi takribani elfu kumi hivi karibuni ambao watatawanywa nchi
nzima ikiwemo mikoa iliyo pembezoni.
Katika
hospitali ya uzazi ya Meta, waziri huyo ameguswa na ufinyu wa wodi za
wazazi na kupelekea mama wajawazito na waliojifungua kulala chini na
wawili wawili kwenye kitanda kimoja na hivyo kuwataka kufanya haraka
ujenzi wa jengo jipya litakaloondoa mrundikano wa mama wajawazito na
watoto njiti.
Hospitali
ya Kanda ya Rufaa Mbeya inakusanya kwa mwezi kiasi cha shilingi Milioni
mia tano na pia inahudumia mikoa saba nchini na kuhudumia zaidi ya watu
milioni mbili.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu
akisalimia na watumishi mara alipofika kwenye hospitali ya rufaa ya
mkoa ya Mbeya.
Waziri Ummy akimsalimia mtoto Jenifer Joel (9) mkazi wa Chunya aliyelazwa hospitalini hapo.
Waziri
wa afya akimjulia hali mtoto Baraka Jekonia (1) mkazi wa Chunya
aliyelazwa wodi ya watoto, Waziri Ummy ameitaka hospitali hiyo kuwachaji
pesa wagonjwa wote wanaofika hospitali ya rufaa moja kwa moja bila
kupatiwa rufaa kutoka vituo vya afya vilivyopo jirani na wananchi ili
kupunguza msongamano kwenye hospitali za rufaa nchini.
Katika
hospitali ya uzazi ya Meta, Waziri Ummy Mwalimu alimsalimia Binti
Kanisia Komba aliyejifungua mtoto wa kike katika hospitali hiyo mama
wajawazito wote wanatibiwa kwa kadi ya bima ya afya inayodhaminiwa
mpango wa kusaidia akina mama wajawazito wa KFW toka Banki ya Ujerumani.
Hospitali
ya Meta tayari imetekeleza maagizo ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu ya kutoa kipaumbele
kwa wazee wote nchini wanapofika kwenye vituo vya kutolea huduma.
Waziri
Ummy akiwasalimia wazazi waliolazwa kwenye moja ya wodi Hospitali ya
Meta kutokana na ufinyu wa wodi inawalazimu akinamama wengine kulala
chini hospitali hiyo inatarajia kuanza ujenzi wa jengo jipya ambalo
litaondoa msongamano wa wazazi hospitalini hapo.
Waziri wa Afya akiwasalimia wagonjwa waliofika Hospitali ya Uzazi ya Meta kupata matibabu.
No comments:
Post a Comment