Waziri Ummy Mwalimu akizungumza na wananchi hao ambao waliomzunguka kutoa kero yao ya kuzuiwa kuendelea na ujenzi wa zahanati.
Wananchi
wa kata ya Ushirika-Tukuyu wakiwa wamebeba bango kuonesha kilio chao
kwa waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto.
Mmoja wa mwanakamati akimueleza mgogoro wao wa eneo la ujenzi wa zahanati kati yao na mkurugenzi wa halmashauri yao.
………………………………………………………………………………………………
Na.Catherine Sungura
Wananchi
wa kata ya ushirika wilayani tukuyu wameusimamisha msafara wa waziri wa
afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto uliokua ukitoka wilayani
kyela kuelekea mbarali kwa madai hawana kituo cha afya wala zahanati
kwa miaka hamsini sasa.
Wananchi
hao ambao walikua wameshika bango kubwa lililoandika hawamtaki
mkurugenzi wa halmashauri hiyo kwa madai ya kuwasimamisha ujenzi mara
mbili
Akieleza
kilio chao katibu.wa kamati ya ujenzi bi.fatma mwandegele alisema eneo
hilo limeingia kwenye mgogoro wa ardhi kwa muda mrefu kati ya kijiji
cha mpunguso na aliyekua katibu tarafa wa kata ya pakati bw.mwakapala
Hatahivyo
alisema kesi kuhusu eneo hilo ilishamalizika na wananchi walikusanya
nguvu zao kwa kuchangia simenti na mawe hata hivyo simenti hiyo
iliharibika
Waziri
Ummy Mwalimu ilimrazimu kwenda kuliona eneo hilo ambalo limechimbwa
tayari kwa kuanza msingi huku mawe yakiwa yamerundikwa pasipo kuendelea
na ujenzi alimuagiza mganga mkuu wa mkoa ambaye alikua nae kwenye
msafara wake,siku ya jumatatu wafike eneo hilo pamoja na mkurugenzi na
mganga mkuu wa wilaya ili waeleze kwanini wasiendelee na ujenzi wa
zahanati hiyo.
“Nawaomba
wananchi muwe watulivu ili tujihakikishie kama kesi hiyo imekwisha na
kwanini tusiendelee na ujenzi huu na jumatatu kabla ya.saa tisa mchana
niwe nimepata ripoti ya eneo hili
Aidha,Waziri
huyo aliwathibitishia wananchi hao kwamba lazima zahanati ijengwe
kwenye kijiji hicho ili kiweze kuwahudumia wananchi na
kuwaahidi.serikali itawaletea wahudumu pamoja na dawa,vifaa na vifaa
tiba.
No comments:
Post a Comment