Kulia Mganga Mkuu mfawidhi wa
hospitali ya Rufaa Iringa dkt Robert Salim, akitoa maelezo ya
uteketezaji wa taka katika hospatali ya Rufaa kwa Naibu Waziri Ofisi ya
Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina na Ujumbe wake
walipokagua mazingira ya hosptali hiyo leo.
Katikati Naibu Waziri Ofisi ya
Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira, Mh luhaga Mpina , kushoto Mkuu wa
Wilaya ya Iringa Bw. Richard Kasesera Kulia Naibu Meya wa mji wa
Iringa Bw. Joseph Liata ambae pia ni diwani (Chadema) kwa pamoja
wakifanya usafi katika soko la mji wa Iringa.
Kushoto Mkuu wa Wilaya ya Iringa
Bw. Richard Kasesera kulia Naibu Waziri Ofisi ya Makmu wa Rais Muungano
na Mazingira Mh Luhaga Mpina wakimwaga maji wakati wakifanya usafi
sokoni Mkoani Iringa Leo.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina, Akiuandaa mche wa mti
kabla kuupanda katika eneo la chanzo cha maji cha chemchem cha Kitwiru,
Leo Mkoani Iringa
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina Akimwagilia maji mara baada
ya kupanda mti , katika eneo la chanzo cha maji cha Kitwiru Mkoani
Iringa.
…………………………………………………………………………………..
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa
Raisi Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina, ameutaka uongozi wa
Hospitali ya Rufaa, Mkoani Iringa Kulitaftia ufumbuzi suala la
uteketezaji wa taka ngumu katika hospitali hiyo.
Mh. Mpina ametoa maagizo hayo leo
alipotembelea Hosptali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa katika ziara yake ya
kukagua usafi wa mazingira na utekelezaji wa sheria ya usimamizi wa
maziringa katika viwanda vya mkoa wa Iringa.
Imeelezwa kuwa uteketezaji wa
tanga hatarishi katika hosptali hiyo ya mkoa umekumbana na changamoto
nyingi ikiwa ni pamoja na kuharibika kwa kifaa cha kuteketeza taka
hospitalini hapo kwa muda mrefu bila matengezo yeyote uliosababishwa na
taratibu za utekelezaji manunuzi serikalini.
Kwa Upande wake mganga mkuu
mfawidhi wa hospital hiyo dkt Robert Salim Amemueleza Naibu waziri Mpina
kuwa taka zizalishwazo katika hosptali hiyo zimekuwa zikitupwa katika
Dampo la mkoani hapo na hata hivyo..hosptali imekuwa na wakati mgumu
sana katika kuteketeza taka hatarishi kama vile za sindano, gloves,
nyembe na bandeji mana haziozi ardhini kirahisi.
Akitolea ufafanunuzi sualala za
uteketezaji wa taka hatarishi hospitalini hapo, mratibu wa kanda ya
nyanda za juu kusini wa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC)
bw. Godlove Mwamsojo..ameleeza kuwa baraza limewahi kushauri uongozi wa
hosptali hiyo kuteketeza taka hizo kwa kusaidiwa na kiwanda cha mbao
cha Sao hill kilichopo wilayani Mufindi kwa kuwa kiwanda hicho kina
vifaa vya kutosha, bila mafanikio kutokana na sababu kwamba hospital
hiyo huzalisha taka nyingi kuzidi uwezo wa kiwanda cha Sao Hill kusaidia
kuziharibu.
Wakati huo huo, Naibu Waziri
Mpina alikagua mazingira ya soko la Mjini Iringa na kushiriki katika
usafi wa mazingira pamoja na kupanda miti, ambapo Mh. Mpina,alipanda
mti katika kata ya Kitwivu na kuwaasa wakazi wa Iringa kuwa walinzi wa
misitu na kutoa taarifa za wizi na uhujumu wa magogo ili sheria ichukue
mkondo wake na kuwaasa watunze vyanzo vya maji kama walivyotunza vizuri
chanzo cha maji ya chemchem cha Kitwivu.
“Taifa lazima lipande miti ili
kuhepukana na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi tunazokumbana
nazo.” Alisisitiza. Aidha Mh Mpina aliiongeza Wilaya ya Mufindi kwa
kupitiliza lengo la kupanda miti milioni moja na laki tano kila mwaka
katika kila wilaya na kupanda miti milioni thelathini na tano kwa mwaka.
No comments:
Post a Comment