Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Tuesday, June 25, 2013

MAHABUSU WAWILI MJINI NJOMBE WATISHIA KUTORUDI GEREZANI MPAKA WAPATE MAELEZO YA KINA KUHUSIANA NA UCHELEWESHWAJI WA UPELELEZI JUU YA KESI YAO,WAHOJI KWA NINI WENGINE WANA KESI KAMA YAO WAACHIWA HURU

  HAPA NI MAHAKAMA YA WILAYA YA NJOMBE MKOANI NJOMBE.

Mahabusu Wawili wa Gereza la Wilaya ya Njombe Jana Walitishia Kutorudi Gerezani Baada ya Kufikishwa Katika Mahakama ya Wilaya ya Njombe na Kuanza Kulalamikia Muenendo wa Kesi Hiyo Kwa Madai ya Kucheleweshwa Kwa Upelelezi Wake Jambo Linalowafanya Kukaa Mahabusu Kwa Muda Mrefu.

Aidha Mahabusu Hao Pia Walimelalamikia Kile Walichokiita Kuwa ni Kubadilishwa Kwa Makosa Yanayowakabili Tofauti na Kile Kinachoelezwa Awali na Badala Yake Wamekuwa Wakibadilishiwa Mashtaka Pindi Wanapofikishwa Mahakamani.

Mbele ya Hakimu ya Mahakama ya Wilaya ya Njombe John Kapokolo,Mahabusu Hao Wamedai Kuwepo Kwa Urasimu Katika Uendeshaji wa Kesi Hizo Kwani Baadhi ya Watu Wamewahi Kufikishwa Mahabusu Kwa Makosa Hayo Lakini Kinachowashangazwa ni Kitendo Cha Mahabusu Hao Kuachiwa Ndani ya Muda Mfupi Huku Wao Wakiendelea Kusota Mahabusu Bila Upelelezi Kukamilika.

Kutokana na Madai Hayo Mahabusu Hao Godfrey Hongori na Eliki Kayage Waliiomba Mahakama Kuwaitia Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya na Mkoa Ili Wawaeleze Kuhusu Malalamiko Yao na Hivyo Wakitishia Kutorudi Gerezani Endapo Ombo Lao Hilo Lisingetekelezwa.

Akijibu Malalamiko Hayo Mahakamani Hapo Mwendesha Mashtaka Serapian Matiku Amesema Watayafikisha Maombi Hayo Kwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa na Wilaya na Ikiwezekana Wafike Kwaajili ya Kuyatolea Ufafanuzi.

Hakimu wa Mahakama Hiyo John Kapokolo Ameahirisha Kesi Hiyo Hadi June 25 na Kusema Kuwa Mahakama Haina Uwezo wa Kujibia Malalamiko Hayo na Badala Yake Wahusika wa Upelelezi Ndio Wanaopaswa Kujibia Suala Hilo.

Wakati Huo Huo Afisa Mtendaji wa Kijiji Cha Kinenulo Wilayani Njombe Donald Mfingwa Amefikishwa Katika Mahakama ya Wilaya ya Njombe na Kusomewa Hati ya Mashtaka Manane Yakiwemo ya Kughushi Stakabadhi na Kujipatia Fedha Kwa Njia ya Udanganyifu Akiwa Mtumishi wa Serikali.

Akisoma Hati ya Mashtaka Mbele ya Hakimu wa Mahakama Hiyo John Kapokoro, Mwendesha Mashtaka Serapian Matiku Ameimabi Mahakama Hiyo Kuwa Mshtakiwa Alitenda Makosa Hayo Kwa Nyakati Tofauti Katika Kipindi cha Mwaka 2012/2013.

Imedaiwa Mahakamani Hapo Kuwa Mnamo Mwaka 2012 Mtuhumiwa Alighushi Stakabadhi na Kujaza Shilingi Elfu Sabini Badala ya Shilingi Laki Moja na Elfu Arobaini.

Amesema Katika kosa la pili  mshtakiwa  anakabiliwa na kosa la  wizi wa fedha taslimu elfu sabini alizoiiba kwa kughushi Stakabadhi ya tarehe 28 mwezi wa 12 mwaka 2012 aliyoitoa kwa Abu na mnamo january 15 ,2013 aliguhi Stakabadhi kwa kuingiza shilingi elfu 15 badala ya elfu 30.

Imeelezwa Mahakamani Hapo Kuwa Mnamo januari 15 mwaka huu aliiba shilingi elfu 15 na januari 19  mwaka huu aliiba shilingi elfu 15 na february 16  mwaka huu aliiba shilingi elfu 10 na mia tano mali ya mwajili wake.

Mwendesha Mashtaka Ameendelea Kuiambia Mahakama Kuwa Katika Kesi Hiyo Upande wa Mashtaka Unatarajiwa Kuwasilisha Mashahidi Wanne na Vielelezo Vitano ambavyo ni barua ya ajira,stakabadhi mbalimbali,kitabu cha makabidhiano,kitabu cha getini na maelezo ya onyo.

Hata Hivyo Mtuhumiwa Amekana Kuhusika na Makosa Hayo na Hakimu Ameahirisha Kesi Hiyo Hadi July 15 Mwaka Huu Itakapoanza Kusikilizwa Mahakamani Hapo

No comments:

Post a Comment