chanzo Francis Godwin blog
Hapa akionekana mwenye uzembe zaidi
Hapa akionyesha majeraha ambayo aliyapata shingoni kutokana na kukabwa shingo na askari huyo
Hapa akiwa hoi kwa kipigo
Bi Rehema Shauri Madongo mkazi wa
Wilolesi mjini Iringa akiwa na mtoto wake baada ya kuponea katika
tundu la sindano kuuwawa kwa kipigo kutoka kwa mmewe ambaye ni askari
polisi mjini Iringa kiasi cha kukimbia nyumba na kurudi kwa wazazi
wake
stepen kanyala akiwa na mke wake siku ya harusi yao iliyodumu kwa miaka mitatu sasa
Bi Rehema akiwa nyumbani kwa wazazi wake baada ya kukimbia nyumba yake kutokana na kipigo kisichokwisha
Mama mzazi wa Rehema akiwa Monica Shauri |
IGP Mwema
WAKATI jeshi la polisi nchini
likiendelea kujiweka karibu na Raia hata kuamua kuanzisha dawati la
jinsia katika vituo vya polisi ,kwa mkoa wa Iringa baadhi ya
askari wanadaiwa kupingana na jitihada hizo za polisi kwa
kushindwa kuheshimu dawati hilo na badala yake kushiriki kulivunjia
heshima jeshi hilo kutokana na kufanya vitendo ambavyo ni kinyume na
mkakati wa jeshi hilo katika kuanzisha dawa.ti la jinsia.
Uchunguzi wa mtandao huu wa
www.matukiodaima.com na www.francisgodwin.blogspot.com umeonyesha kuwa
dawati hilo kwa askari limekosa kuheshimika kutokana na vitendo vya
unyanyasaji wa kijinsia ambavyo baadhi ya askari (30) wamekuwa
wakifanya kwa watoto wao na wake zao.
Rehema Shauri Madongo ni mmoja kati
ya mwanamke ambaye amebahatika kuolewa na askari polisi kitendo cha
upelelezi ambaye anaeleza jinsi alivyotendewa vitendo vya ukatili wa
kijinsia kwa kuteswa na kupigwa kikatili na pindi anapofika polisi
hakuna hatua zozote zinazochukuliwa kwa mtuhumiwa huyo ambaye ni
askari .
" Mimi niliolewa kwa ndoa na Stephen
Kanyala ambae ni askari kitengo cha upelelezi ila baada ya kuolewa
ukiwa umepita mwezi mmoja tuo nilianza kushuhudia mateso ya ndoa
kutokana na kipigo na mateso makali niliyokuwa nikiyapata"
Anasema kuwa kila wakati pindi
anapotaka kujua jambo kutokana kwa mume wake huyo hasa pale
anapoona jumbe zenye utata katika simu yake ambazo zimetoka kwa
wanawake anaiowatambua vizuri amekuwa akijibiwa kwa kipigo kikali.
Rehema alisema kuwa ni rahisi kwake
kuweza kuhesabia siku ambazo hajapigwa kuliko kuhesabi siku ambazo
amepigwa ambazo ni nyigi zaidi .
Kwa alisema toka ameolewa kila mara
amekuwa akipokea kipigo na mbaya zaidi kabla ya kupigwa amekuwa
akifungwa mikono kwa pingu zinazotumika kuwafunga watuhumiwa pingu
ambazo mume wake huyo amekuwa akizihifadhi ndani ya nyumba .
" Kweli inasikitisha sana kusimulia
kwani kabla ya kupigwa nimekuwa nikifungwa pingu mikono kama mharifu
sugu na baada ya hapo kipigo kikali kimekuwa kikinikuta ....hadi
sasa nimepigwa zaidi ya mara 20 na polisi nimekwenda kuripoti
mara tatu na Hospital nimelazwa mara moja ila siku nyingine nimekuwa
nikiugulia nyumbani ila nyumbani kwa wazazi nimerudi mara tatu sasa"
Alisema kuwa mbali ya kupigwa na
kuumizwa ila kuna mateso mengine ambayo amekuwa akiyapata kutoka kwa
mwanaume huyo ni siri yake na hayapaswi kuelezwa hapa kutokana na
jinsi ambavyo askari huyo anavyomtenda ukatili wa kinyama.
Hata hivyo alisema kuwa akiwa na mimba
ya mwezi mmoja hali ya kipigo ilizidi zaidi na wakati mwingine
alipata kumfunga shingo na kanga kwa kutaka kunyonga shingo huku
akitishi kumuua .
Alisema kuwa baada ya kujifungua
mtoto wa njia ya Oparesheni mwanaume huyo alimpiga kiasi cha kumjeruhi
mtoto wa mwezi mmoja kwa kumpiga kofi ambalo lilielekezwa kwake na
bahati mbaya likaishia kwa mtoto.
Aidha alisema kuwa kila akifika
polisi kufungua kesi hakuna utekelezaji unaofanyika kutokana na
polisi kulindana na kuwa suala hilo la askari polisi kulindani
lilianza toka wakati kamanda wa polisi akiwa Evarist Mangala ,pia
alipofika kamanda Michael Kamuhanda ambaye kwa sasa amehamishwa baada
ya cheo kupanda pia amepata kufikisha malalamiko yake ila hakuna
jipya ila sasa amefikisha tena suala hilo kwa kamanda mpya RPC
Ramadhan Mungi ambae amedai kuwa na imani nae zaidi katika kulishughulikia suala lake
Pia alisema mbali ya
kupigwa akiwa nyumbani kwake ila bado anapoamua kukimbia nyumba hiyo
na kukimbilia kwa wazazi wake bado askari huyo amekuwa akimfuata
na kumpa kipigo mbele ya wazazi wake .
Hivyo alisema katika kunusuru uhai wake kwa sasa ameamua kurudi kwa wazazi wake na suala la ndoa hataki tena .
Kwa upande wake Mama mzazi wa
Rehema akiwa Monica Shauri alisema kuwa amechoka kuuguza binti yake
kwa kipigo na kuwa kuna wakati mwanaume huyo amekuwa akitishia
kumpiga hata yeye.
Hivyo alisema kwa sasa mbali ya kumtoa
binti yake Hospital ila wamekuwa wakiishi ndani wamejifungia milango
kuogopa askari huyo kuja kuwafanyia ukatili ikiwa ni pamoja na kuwaua
kwa risasi kama ambavyo amekuwa akiwatisha mara kwa mara kuwa dawa yao
inachemka na ipo siku wataonja mauti.
Bi Shauri alisema mbali ya kuwa yeye ni
mmoja wa wacha Mungu kwa maana na Mlokole mzuri ambae kila wakati
asubuhi lazima aende kusali ila kwa sasa anaogopa kutoka asubuhi kwa
kuhofia kuvamiwa na askari huyo .
Hivyo aliomba jeshi la polisi kuweza
kumpa ulinzi yeye na familia yake ama kumkamata mtuhumiwa huyo ambae
inadaiwa kwa sasa yupo katika mji wa Iringa ila askari wenzake
wanamlinda.
Kuhusu uamuzi wa binti yake wa kuomba
ndoa hiyo kuvunjwa alisema anaungana na binti yake kuikataa ndoa hiyo
na kuwa kwa sasa wapo tayari kurudisha mahali yake ya Tsh 200,000
ambazo alizitoa kama mahali ili kunusuru uhai wao na uhai wa mtoto
wake huyo.
No comments:
Post a Comment