Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Tuesday, May 19, 2015

RC NJOMBE AFUNGUA JENGO LA CHEKECHEA MTAA WA JOSHONI LILILOJENGWA NA WANANCHI PAMOJA NA WADAU WA ELIMU



 DIWANI WA KATA YA MJIMWEMA JIMMY NGUMBUKE WA UPANDE WA KULIA



 WANANCHI JOSHON WSAKISIKILIZA HOTUBA YA MGENI RASMI





 DC NJOMBE SARAH DUMBA AKIKATA UTEPE WA JENGO HILO  LA CHEKECHEA

 BAADA YA KUFUNGUA JENGO AKISAINI KITABU CHA WAGENI




 AKIZUNGUMZA KWA NIABA YA MKUU WA MKOA WA NJOMBE DKT REHEMA NCHIMBI,MKUU WA WILAYA  YA NJOMBE BI.SARAH DUMBA AKITOA HOTUBA YAKE KWA WANANCHI WA JOSHON





 


Mkuu Wa Mkoa Wa Njombe Dkt Rehema Nchimbi Amezindua Jengo La Wanafunzi Wa Chekechea   Lenye Vyumba Vitatu  Vya Madarasa Na Ofisi Moja Ya Walimu Lililopo Katika Mtaa Wa Joshoni  Ambalo Limegharimu  Zaidi Ya Shilingi  Milini 17  Na Laki 4  Ambapo  Jengo Hilo Linakabiliwa Na Changamoto Ya Kukosekana Kwa Vyoo Na Madawati.

Akizungumza  Wakati Wa Uzinduzi Wa Jengo Hilo  Kwa Niaba Ya Mkuu Wa Mkoa Wa Njombe Dkt Rehema Nchimbi,Mkuu Wa Wilaya Ya Njombe Bi. Sarah Dumba  Pamoja Na Kupongeza Wananchi Wa Mtaa Wa Joshoni  Kwa Kushiriki Kikamilifu  Uchangiaji Wa Michango Kwaajili Ya Ujenzi Wa Jengo Hilo Pia Amewataka Kuendelea Na Moyo Huyo Wa Kufanya Maendeleo  Ya Mtaa  Kwa Manufaa Yao.

Aidha Bi.Dumba Amesema Kuwa Wananchi Wa Mtaa Huo Wanatabia Nzuri Ya Kuhitaji Maendeleo  Na Kusema Kuwa Waepukane Na  Malumbano Ya Kisiasa  Wakati Wa Kutekeleza Miradi Ya Serikali  Huku Akiwataka Kushirikiana Na Halmashauri  Ya Mji Wa Njombe  Ili Kuwapata Walimu Wa Chekechea Ambao Wamesomea  Na Kwenda Kuwaajiri Katika Shule Hiyo .

Katika Hatua Nyingine  Bi. Dumba  Ametaka Serikali Ya Mtaa Kutoruhusu  Shughuri Nyingine Kufanyikia Katika Eneo La Shule Hiyo Ya Chekechea  Ikiwemo Kuanzisha Masomo Ya Ziada  Yaani Tuisheni  Pamoja Na Mikutano Yoyote Ya Kisiasa  Isipokuwa Mikutano Ya Serikali Ya Mtaa Ambayo Inalenga  Maendeleo  Ya Elimu Kwa Watoto Pamoja Na Afya Na Maendeleo Ya Mtaa Huo.

Akisoma Risala Fupi Kwa Mgeni Rasmi Afisa Mtendaji Wa Mtaa Wa Joshoni Bwana  Richard Mwihechi Amesema Kuwa Jengo Hilo Limeanza Kujengwa Tangu  Septemba  2014  Kwa Kushirikiana Na Wadau Mbalimbali Wa Elimu  Pamoja Na Halmashauri Ambapo  Jumla Ya Fedha Taslimu Ni Shilingi Milioni 13 Laki Tatu Na Sitini Elfu Ikiwa Ni Michango Toka Kwa Wananchi Na Wadau.

Bwana Mwihechi  Amesema Kuwa  Pia Kuna Wadau Wa Elimu Waliochangia Michango Ya Vifaa   Ikiwemo Mchanga Na  Kifusi  Vyenye Thamani Ya  Ya Zaidi Ya Shilingi Milioni  Moja Na Laki Sita  Na Kufanya Kiasi Cha Zaidi Ya Shilingi  Milioni 17 Ya Fedha Zilizotumika    Pamoja Na Michango Inayoendelea  Kuchangishwa Kwa Wananchi Huku Changamo Ikiwa Ni Kukosekana Kwa Vyoo,Uzio Na Madawati Yenye Thamani Zaidi Ya Shilingi Milioni 20. 

No comments:

Post a Comment