Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Tuesday, May 19, 2015

BASI LA LUWINZO JUZI MEI 17 LILIPATA AJALI MBAYA NA KUSABABISHA MAJERUHI WALIOPELEKWA HOSPITALI YA KIBENA HALI ILIKUWA HIVI


 BASI LA LUWINZO LA KUTOKA DAR ES SALAAM KWENDA NJOMBE  LIKIWA LIMEPINDUKA BAADA YA KULIGONGA GARI LILILOKUWA MBELE YAKE AINA YA FUSO


 HUKU NDIKO  BASI HILO LA LUWINZO LILIKOKUWA LIMEDONDOKA  BAADA YA KUGONGA  FUSO  KWA NYUMA ILIYOKUWA MBELE YAKE
 HILI NI GARI AINA YA FUSO  LIKIWA LIMEDONDOKA BARABARANI BAADA YA KUGONGWA KWA NYUMA NA  BASI LA LUWINZO NA MASHUHUDA WAKIENDELEA KUSHUHUDIA KILICHOTOKEA



 MAAFISA USALAAMA WA BARABARANI WAKIFANYA KAZI YAO YA UKAGUZI NA KUIMARISHA USALAAMA  ENEO LA TUKIO








 HILI NI LUWINZI LIKIWA POLISINI BAADA YA KUPINDUKA NA KUACHA NJIA
 HILI NI GARI AINA YA FUSO LIKIWA BARABARANI
 HILI NI GARI AINA YA FUSO  AMBALO LILIKUWA MBELE YA BASI  LA LUWINZO




 Na Michael Ngilangwa- Njombe
Majeruhi Watano Wa Basi La Luwinzo Na  Gari La Mizingo Aina Ya Fuso  Wamepelekwa Katika Hospitali Ya Kibena Kwaajili Ya Matibabu Baada Ya Kutokea Kwa Ajali Mbaya  Iliyotokea Majira Ya Saa Kumi Na Moja Eneo La Mashamba Ya Kampuni Ya Tanwat Karibu Na Kibao Cha Namba 3 Iliyotokea Majira Ya Saa Kumi Na Moja Jioni.

Ajali Hiyo Imelikutanisha Gari La Luwinzo  Aina Ya Scania Lenye Namba Za Usajiri T 853 AUA  Ambalo Lilikuwa Likitokea Dar Esalaam Kuelekea Njombe Kuligonga Kwa Nyumba Gari Lililokuwa Mbele Yake  La Mizigo Ambalo Lilikuwa Limechukua Mchanga  Likitokea Makambako  Kuelekea Makete   Lenye Namba T 899 AWK  Mali Ya Patrick Sanga  Na Kusababisha Ajali Hiyo  Baada Ya Magari Hayo Kupinduka.

Wakizungumza Na Uplands Fm  Baadhi Ya  Mashuhuda Na Abiria Waliokuwa Kwenye  Gari La Luwinzo Wamesema Kuwa Chanzo Cha Ajali Hiyo Ni Mwendo Kasi Aliokuwa Akiendesha  Dereva Wa Basi La Luwenzo   Ambaye Alitaka Kulipita Gari La Mizigo  Huku Anatambua Kuwa Barabara Ni Ndogo Na Kuligonga Gari La Mizigo  Lililokuwa Mbele Yake Na Hatimaye Magari Yote Kuacha Njia  Na Kupinduka.

Akizungumza Akiwa Eneo La Tukio Dereva Wa Gari Lililogongwa Kwa Nyuma  Justine Malekela  Amesema  Tatizo La Basi Hilo Kumgonga Kwa Nyuma Ni Baada Ya Kutaka Kulipisha Gari Lililokuwa Mbele Yake Alafu Akabadilisha Mawazo Na Kurudi Kwenye Saiti Ya Ikiwa  Gari Lake Likiwa  Kwenye Mwendo Kasi Na Kuligonga Gari Lake Ambalo Ni Fuso  Huku Kijana Wa Gari La Luwinzo Akisema Luwinzo Halikuwa Likienda Kwa Mwendo Kasi Lilikuwa Speed 80.

Kwa Upande Wake Muuguzi Wa Kibena  Bi. Agnes Kihele Akizungumza  Kwa Niaba Ya Muuguzi Mkuu Ambaye Amedaiwa Kupata Dharula Na Kwenda Nyumbani  Kwake Wakati Mwenzake Wa Kumpokea Akiwa Hajafika Amesema Amethibitisha Kupokea Majeruhi Watano Ambao  Bado Wanaendelea Kupata Matibabu Huku Wengine Wakifungiwa Vidonda Na Kuhuhuwa Kwenda Nyumbani Kwao.

Matukio Ya Ajali Nchini Yameendelea Kujitokeza  Maeneo Mbalimbali Na Kupoteza Ndugu Na Jamaa Huku Watumishi Wa Mungu Wakiendelea Kuiombea  Nchi Ispatwa Na Matukio Hayo Na Kuwasihi Madereva Waendeshe Kwa Mwendo Wa Taratibu   Ili Kunusuru Roho Za Watanzania.


No comments:

Post a Comment