hili jeshi la Polisi kutoka kituo cha makambako kikiwa kwenye msafara wa Chadema katika kata ya Mahongole Leo.
Huyu ni Mzee Mfumbirwa aliyekamatwa na
Mwenyekiti wa kijiji cha Manga na kisha kupigwa na Kuvuliwa nguo zote
akiwa kiongozi wa CHADEMA Kijijini humo,
CHADEMA Wasema watafungulia kesi ya udhalilishaji Mwenyekiti huyo.
Siasa zilikuwa zikiendelea hapa.
Hali ya hewa katika kata ya Mahongole ni mbaya kuliko kawaida ukame waanza kutanda na mimea imeanza kukauka.
Huyu ni Kaimu katibu wa Chadema wilaya ya
Njombe Alatanga Nyagawa akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Mahongole
leo wakati wa mkutano wa CHADEMA.
Wananchi na wafuasi wa Chadema wakiwa wamenyoosha mikono juu kupinga suala la kufeli kwa wanafunzi wa Kidato cha Nne.
Wananchi wa kijiji cha Mahongole wakitawanyika mara baada ya kuisha kwa mkutano kijijini humo leo
Mzee Mfumbirwa Kamanda wa CHADEMA kijiji cha Manga akifurahia kufika kwa makamanda wa CHADEMA toka mkoani leo na kufanya mkutano mkubwa kijijini kwake.
Maneno
yalikuwa yakiendelea kwa wakazi wa Kihanga kijiji cha Manga kata ya
Mahongole katika Halmashauri ya mji wa Makambako Mkoani Njombe leo.
Chama cha aDemokrasia na Maendeleo CHADEMA Mkoani Njombe jana kimeendelea na mikutano yake ya kuzungumza na wananchi kwenye maeneo mbalimbali huku wakiitaka serikali kuweka bayana taarifa za shughuli za maendeleo vijijini.
Mikutano hiyo kwa siku ya jana imeendelea katika
vijiji vya Mahongole
na Kihanga kata ya Mahongole huku suala la kufeli kwa mitihani ya
kidato cha Nne likionekana kuwa kikwazo kwa wananchi wengi vijijini
humo.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Kihanga na Mahongole
wamelalamikia tatizo la serikali kushindwa kukidhi haja ya wananchi wake
hususani katika sekta ya Afya pamoja na elimu huku mitihani ya kidato
cha Nne likionekana kuwasumbua wengi.
Aidha wamelalamikia kitendo
cha kushindwa kusomewa taarifa za mapato na matumizi ya kijiji kwa
kipindi kirefu zikiwemo fedha za michango ya ujenzi wa shule kiasi cha
shilinvgi Elfu kumi.
David Tweve maarufu kama mzee Nyalembe ni
mhasibu wa Chadema Jimbo la Njombe kaskazi anajitokeza na kuzungumzia
juu ya kushuka kwa elimu ya Tanzania na kuwatupia lawama viongozi wa
serikali kwa kujenga shule nyingi za kata bila kuboresha miundombinu ya
kutosha.
Akiwa
katika kijiji cha Kihanga baada ya kuhitimisha mkutano katika kijiji cha
Mahongole kaimu katibu wa Chadema wilaya ya Njombe bwana Alatanga
Nyagawa amesema kuwa bila mabadiliko ya kweli nchi hii haiwezi kunyooka
ikiwa ni pamoja na kulaani tabia za baadhi ya viongozi wa kata na vijiji
hivyo kwa kushindwa kusimamia serikali hiyo.
Hata hivyo amesema
kuwa kitendo cha serikali kuwahamisha viongozi wabadhilifu na kuwapeleka
kituo kingine ni kuendelea kufuga wezi katika nchi.
No comments:
Post a Comment