Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe
akizungumza na Wadau wa Sanaa (hawapo pichani) kuhusu nini kifanyike kwa
mavazi ya wasanii sababu ya kuwepo kwa wasanii wengi wanaovaa mavazi
yanayokiuka na maadili ya kitanzania katika kikao chake na wadau
mbalimbali wa Sekta ya Saana nchini kilichofanyika leo jijini Dar es
Salaam, kutoka kushoto ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bibi.
Joyce Fissoo na Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA)
Godfrey Mngereza (kulia).
Katibu
Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo (kushoto) akitoa
ufafanuzi kwa wadau wa Sanaa (hawapo pichani) kuhusu Sheria ya Filamu
nchini inayosema lolote linalotoka nje ya nchi,Michezo ya kuigiza na
kazi yoyote ya kisanii inayotengenezwa hapa nchini kusawili hali halisi
ya kitanganyika, katika kikao kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam na
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe
(Kulia) kujadili nini kifanyike kutokana na kuwepo na mmomonyoko wa
maadili katika mavazi kwa wasanii.
Katibu
wa Shirikisho la Muziki Tanzania ambaye ni Mwanamuziki Mkongwe John
Kitime akisisitiza kuwepo kwa Kampeni ya Kitaifa kusisitiza suala la
mavazi yenye kulinda utamaduni wetu katika kikao kilichofanyika leo
jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.
Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) kujadili suala la mavazi kwa
wasanii na taifa kwa ujumla.
Mwanamuziki
wa Bongo Fleva nchini Stara Thomas akichangia mada ya kuhusu mavazi ya
heshima kwa wasanii nchini katika kikao kilichofanyika leo jijini Dar es
Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison
Mwakyembe (hayupo pichani).Na Anitha Jonas – WHUSM
No comments:
Post a Comment