Mkuu
wa Wilaya ya Gairo, Siriel Shaidi Mchembe amezindua kampeni ya kupanda
miti Kata kwa Kata. Akizungumza jana wakati akizindua kampeni hiyo
iliyofanyika katika tarafa la Nongwe kata ya Chanjale, alisema kuwa
wananchi ni lazima waheshimu kuhifadhi mazingira kwa kupanda miti na si
kuikata ovyo.
Katika
kampeni hiyo Mhe. Siriel aliambatana na Meneja wa Misitu Wilaya Bw.
David Maiba waliweza kuwahamasisha wananchi kupenda mazingira maana
ndiyo yamekuwa yakisababisha wao kupata nvua. "Nawaomba wananchi mpende
kuhifadhi mazingira maana ndiyo uhai wetu ambao unasababisdha hata mvua
kupatikana, sehemu ikiwa jangwa hamuwezi pata hata maji, niwaombe sana
mtunze mazingira kwa ukaribu sana," alisema mhe. Siriel. Kampeni hiyo
imeanzia Tarafa ya Nongwe Kata ya Chanjale. Tarafa hii ipo uwanda wa juu
ambapo mvua tayari zimeanza.
Viongozi
wengine ambao aliambatana nao ni Diwani wa Chanjale Mhe. Maswaga
Malima, Mtendaji Kata Bi. Stella Ngomano, Wenyeviti wa Vijiji, Watendaji
wa Kata, Wazee Maarufu, Viingozi wa Dini na wananchi kwa ujumla. Kata
ya Chanjale ina Misitu ya Hifadhi yenye ukubwa wa ekari 3,000. Aliongeza
kuwa upandaji wa miti utakuwa ni zoezi endelevu na ameshaagiza kila
kijiji kiwe na kitalu cha kuzalisha miti japo changamoto inayowakabili
ni viriba, ambapo wanahitaji viriba zaidi ya milioni moja kwa Wilaya
yote ya Gairo.
Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Shaidi Mchembe akizungumza machache na wananchi waliofika katika uzinduzi huo.
Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Shaidi Mchembe akipanda miti kuashiria uzinduzi wa kampeni hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Shaidi Mchembe akielekea eneo la tukio na wananchi eneo la tukio.
No comments:
Post a Comment