Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Friday, December 15, 2017

Mabondia Francis Cheka na Shabani Kaoneka wapima uzito leo,kuzichapa kesho uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara


Mabondia Francis Cheka na Shabani Kaoneka, wamepima uzito leo tayari kwa pambano lao linalotarajiwa kufanyika kesho Jumamosi katika uwanja wa Umoja  Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara, ambapo Francis Cheka anatetea mkanda wake wa IBO Africa

Zoezi la upimaji Uzito likiwa linaendelea na kusimamiwa na Mwenyekiti wa kamati ya waamuzi wa Ngumi za Kulipwa Tanzania Ally Bakari na kuthibitisha Ulinganifu wa Uzito.

Mara baada ya zoezi Hilo Franciss Cheka ambaye anatetea Mkanda IBO Afrika amewaomba mashabiki wa ngumi Mkoa wa Mtwara Kuweza kujitokeza kwa wingi na tayari amefanya mazoezs ya kutosha Kuweza kushinda

Pambano hilo la round Kumi, litasindikizwa na mapambano ya utangulizi yatakayowahusisha mabondia wa Mtwara dhidi ya mabondia kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro na Tanga sambamba na burudani ya muziki kutoka kwa wasanii Sholo Mwamba na 20 Percent.
 
 

No comments:

Post a Comment