Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan
MAKAMU
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan
anatarajiwa kufungua kambi ya uchunguzi wa macho, kisukari na shinikizo
la damu.
Kambi
hiyo ya siku tatu imeandaliwa kwa pamoja kwa kushirikiana na Klabu ya
Lions ya Dar es Salaam (Host), kwa kushirikiana na Hospitali ya Regency
ya jijini hapa.
Kambi hiyo itakuwa bure kwa wananchi wote watakaojitokeza kuanzia siku ya Ijumaa katika Wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.
Kwa
mujibu wa taarifa ya Lions Klabu iliyotolewa na Mwenyekiti wa Hospitali
ya Regency Dk. Rajni Kanabar, ufunguzi rasmi wa kambi hiyo utafanyika
siku ya Jumamosi na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa
kuwa mgeni rasmi.
Kambi
hiyo itafanyikia kwenye kiwanda cha KNAUF Gypsum Wilaya ya Mkuranga,
Kata ya Vikindu kijiji cha Kisemvule Mkoa wa Pwani kuanzia siku ya
Ijumaa wiki hii.
Alisema kambi hiyo ya bure ya siku tatu itaanza tarehe 27 hadi 29 mwezi huu
Dk. Rajni Kanabar, aliwataka wananchi wa Mkoa wa Dar es salaam na Pwani kujitokeza kwa wingi kuchangamkia fursa hiyo.
Alisema
Lions Klabu ya Lions imeamua kuandaa kambi hiyo ya bure baada ya
kubaini kuwa kuna wananchi wengi wanasumbuliwa na maradhi hayo lakini
wanakosa uwezo wa kwenda kupima.
“Hii
ni fursa adimu watu wajitokeze kwa wingi kuja kupima afya zao bure,
huduma hiii itatolewa kwa muda wa siku tatu mfululizo kuanzia siku ya
Ijumaa hadi Jumapili hivyo wananchi wote wachangamkie hii fursa,”
alisema.
Klabu
ya Lions ya Dar es Salaam (Host), imekuwa ikiandaa kambi ya uchunguzi
mbalimbali kila mwaka ambapo wananchi hupata fursa ya kwenda kupima
bure.

No comments:
Post a Comment