Msajili
wa vyama vya Siasa Mhe. Jaji Francis S.K Mutungi akisisitiza jambo kwa
watumishi (hawapo pichani) wakati wa Mafunzo ya siku mbili ( jana na
leo)kwa watumishi watakaoshiriki katika usimamizi wa utekelezaji wa
matakwa ya Sheria ya Gharama za Uchaguzi kwa Vyama vya Siasa na
wagombea yaliyofanyika katika ukumbi wa Bunge Jijini Dar esa Salaam.
Bi
Piencia Kiure, Msajili Msaidizi akitoa maada juu ya Elimu ya Maadili ya
Vyama vya Siasa wakati wa Mafunzo ya siku mbili ( jana na leo)kwa
watumishi watakaoshiriki katika usimamizi wa utekelezaji wa matakwa ya
Sheria ya Gharama za Uchaguzi kwa Vyama vya Siasa na wagombea
yaliyofanyika katika ukumbi wa Bunge Jijini Dar esa Salaam.
Bi.
Esther Mwanri, Mwanasheria Mwandamizi aktoa mada juu ya matendo
yaliyokatazwa kwenye sheria ya Gharama za Uchaguzi wakati wa Mafunzo ya
siku mbili ( jana na leo)kwa watumishi watakaoshiriki katika usimamizi
wa utekelezaji wa matakwa ya Sheria ya Gharama za Uchaguzi kwa Vyama
vya Siasa na wagombea yaliyofanyika katika ukumbi wa Bunge Jijini Dar
esa Salaam.
Na Monica Laurent, Ofisi ya Msajili wa Vyamavya Siasa
Msajili
wa Vyama vya Siasa nchini Mhe. Jaji Francis S.K Mutungi amewataka
watumishi kutoka ofisi yake kuhakikisha wanafanya kazi kwa kuzingatia
sheria na kanuni za nchi ili kuleta weledi katika kazi.
Hayo ameyazungumza wakati akifungua mafunzo ya siku mbili yaliyoandaliwa
kwa ajili ya watumishi watakaoshiriki katika usimamizi wa utekelezaji
wa matakwa ya Sheria ya Gharamaza Uchaguzi kwa Vyama vya Siasa na
wagombea yaliyofanyika Jana na Leo katika ukumbi wa Bunge Jijini Dar esa
Salaam.
“Chapeni
kazi na kuwa vinara wa kusimamia gharama za uchaguzi na maadili ya
Vyama vya Siasa ili kubaini wagombea ambao hawafuati matakwa ya
sheria ” amesisitiza Jaji Mtungi.
Naye Bi Piencia Kiure, Msajili Msaidizi wakati akitoa mada juu Elimu ya
maadili ya Vyama vya Siasa ,amewasisitiza watumishi kuendelea na
utamaduni wa kufanya kazi kwa weledi.
Sheria
namba 6 ya Gharama za Uchaguzi ya mwaka 2010 iliyofanyiwa marekebisho
mwaka 2015 kupitia Amri ya Gharama ya uchaguzi inaweka wazi viwango vya
juu vya matumizi kwa wagombea, kudhibiti matumizi ya fedha zinazotumika
wakati wa uchaguzi kuanzia katika mchakato wa uteuzi, kampeni na kupiga
kura ili kuweka uwanja sawa wa kisiasa na kudhibiti vitendo vya rushwa.
Sheria
hii hubainisha wajibu wa Mgombea na Chama cha Siasa kujaza fomu maalumu
za gharama za uchaguzi ili kubainisha bajeti yake ambayo ni mapato na
vyanzo vya mapato na kurejesha katika ofisi ya Msajili wa Vyama vya
Siasa ndani ya siku saba baada ya uteuzi wa wagombea unaofanywa na Tume
ya uchaguzi .
Fomu
maalumu ya kubainisha marejesho ya matumizi ya uchaguzi inayoambatana
na kumbukumbu na stakabadhi za malipo hujazwa na mgombea na kurejeshwa
kwenye chama chake ndani ya siku sitini baada ya uchaguzi, chama cha
siasa kina wajibu wa kuiwasilisha fomu hiyo kwenye ofisi ya Msajili wa
Vyama vya siasa ndani ya siku 180 baada ya kutangazwa kwa matokeo ya
uchaguzi.
Hata
hivyo ukiukwaji wa sheria hii unaambatana na adhabu kali ambayo hutolewa
kwa chama ambacho kitashindwa kuwasilisha mapato na matumizi ya kila
mgombea ambayo ni pamoja na kufutiwa kushiriki uchaguzi endapo
kitashindwa kutoa maelezo ya kuridhisha.
Usimamizi
wa Sheria ya gharama za Uchaguzi katika uchaguzi mdogo wa madiwani
unaotarajiwa kufanyika tarehe Novemba 26 mwaka huu ni mwendelezo wa
usimamizi wa sheria hii ambao hufanywa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya
Siasa wakati wa uchaguzi wa Urais, Wabunge na Madiwani. Kwa mara ya
kwanza sheria hii ilianza kutumika katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2010
No comments:
Post a Comment