Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
jana alifungua Tamasha la Wasanii Wanawake wa mkoa wa Kusini Unguja.
Tamasha
hilo lililofanyika kwenye ukumbi wa Coco Blue ,Jambiani na kuhudhuriwa
na Viongozi mbali mbali wa Chama na Serikali pamoja na wananchi wa mkoa
wa Kusini Unguja.
Makamu wa Rais aliwashukuru Waandaaji wa Tamasha hilo ambao wamesaidia kuwaleta wanawake wa mkoa wa Kusini pamoja.Makamu
wa Rais amewapongeza wanawake wa mkoa wa Kusini kwa kuwa wa kwanza
kutekeleza wazo lililowazwa na kuonyesha utamaduni wa Kusini.
Mhe.
Samia alisema Utamaduni wa zamani hauna budi kuendelezwa ili vijana wa
sasa wajue wapi tumetoka, wapi tulipo na wapi tunaelekea.Akivitaja
baadhi ya vitu alivyoviona kwenye ufunguzi huo kama Manda, Mabobwe
,Vipopoo, ngoma ya Msanja ambavyo kwa pamoja vina lengo la kuleta yale
mazuri ya zamani ambayo yametutoka.
Alisema
Vijana wengi hawajui Kiwe-jiwe la kusagia chakula (Blender za Bibi
zetu) wao wanajua Blender, hivyo ni vyema Tamasha hili likaja na vitu
vingi mwakani waelewe hata maji tuliyatunza kwenye Mtungi ambao wao kwa
sasa wanayajua Majokofu.
Hivyo
aliwasihi Wanawake wa kusini kufufua tamaduni zetu na kuzidumisha,
alisema sema yeye anatoka Kizimkazi ambapo ngoma maarufu ni Shomoo na
Dandaro .Makamu
wa Rais alisema kuwa Utamaduni utasaidia kuwafunza watoto wetu
uzalendo,mazingira, nidhamu ya maisha kwani utamaduni unajumuisha kila
kitu kuanzia chakula, mavazi, vifaa vilivyotumika,filamu, ngoma na
burudani mbali mbali.
Mhe.
Samia aliwapongeza sana wanawake wa mkoa wa Kusini kwa kutoka kwenye
utamaduni wa kukaa tu na badala yake kufanya shughuli zinazowaingizia
kipato. “Nimefurahishwa kuona wakina Mama sasa hivi wanatoka wana
Vikundi vya Kulima tumeonyeshwa wanalima Tungulee, wanalima
Karoti,wanalima michicha hii yote ni utamaduni kwamba tumetoka kwenye
utamaduni wa kukaa tu na kusubiri bwana haji lakini sasa tunatoka
tunajituma na sisi tunapata mapato yetu tunaendelea na maisha yetu”
Makamu
wa Rais alisema ni wajibu wa kila mama kutunza na kufundisha watoto
wetu Tamaduni zetu, “Tunautamaduni ambao hautakiwi kuonyeshwa mbele za
watu na ule nao tufundishe watoto wetu, tusiuache , tunakuwa wa kisasa
mno , tunajifanya wa kisasa mno kiasi ambacho mambo mengine tunayaacha
lakini ambao kwa sie tuliofanyiwa huko nyuma unajua faida yake na watoto
wetu wanaokosa kufanyiwa sasa hivi tunaona hasara yake”
Mwisho
Makamu wa Rais alitoa rai kwa waandaaji wa Tamasha hilo kuhakikisha
linafanyika kila mwaka na kujumuisha tamaduni mbali mbali zenye lengo la
kujenga na kuimarisha mshikamano pamoja na kudumisha upendo na amani
katika jamii, aliwashukuru wadhamini waliosaidia kufanikisha Tamasha
hilo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. SAMIA SULUHU HASSAN
akiangalia kofia iliofumwa kwa mikono wakati wa uzinduzi wa Tamasha la
Wasanii Wanawake wa mkoa wa Kusini Unguja uliofanyika jana kwenye ukumbi
wa Coco Blue Jambiani.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Tamasha la Wasanii Wanawake wa
Mkoa wa Kusini Unguja liliofanyika jana kwenye ukumbi wa Coco Blue,
Jambiani.

Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akihutubia wakati wa ufunguzi wa Tamasha la Wasanii Wanawake wa Mkoa wa
Kusini Unguja liliofanyika kwenye ukumbi wa Coco Blue, Jambiani.


No comments:
Post a Comment