Kwa
upande wao Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) kupitia kwa
Mwakilishi wao nchini,Chansa Kapaya, wameahidi kushirikiana na Serikali
ya Tanzania kuhakikisha wakimbizi wa Burundi 6,800 walioomba kurejea
nchini kwao wanasahiliwa na kurejeshwa kwao katika hali ya utu na
usalama huku shirika hilo likizishukuru Serikali za Tanzania na Burundi
kwa msaada wao walioupata katika kushughulikia masuala ya wakimbizi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani na Elimu ya Uzalendo kutoka nchini Burundi, Pascal
Barandagiye, akibadilishana nyaraka na Mwakilishi wa Shirika la
Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) nchini Tanzania, Chansa Kapaya
(kulia) zenye makubaliano juu ya Mpango wa Kuwarejesha Wakimbizi wa
Burundi wanaohifadhiwa mkoani Kigoma.Katikati ni Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba.Makubaliano hayo yamefanyika mwishoni mwa
wiki, Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, jijini Dar es
Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Wajumbe
kutoka Serikali ya Burundi wakiongozwa na Balozi wa Burundi nchini
Tanzania,Gervais Abayeho wakiwa katika Mkutano wamakubaliano juu ya
Mpango wa Kuwarejesha Wakimbizi wa Burundi wanaohifadhiwa mkoani
Kigoma.Makubaliano hayo yamefanyika mwishoni mwa wiki,Ukumbi wa
Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.Picha na
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Wajumbe
kutoka Mashirika mbalimbali ya kimataifa wakiwa katika Mkutano wa
makubaliano juu ya Mpango wa Kuwarejesha Wakimbizi wa Burundi
wanaohifadhiwa mkoani Kigoma.Makubaliano hayo yamefanyika mwishoni mwa
wiki, Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, jijini Dar es
Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba,akibadilishana nyaraka na
Mwakilishi wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) nchini
Tanzania,Chansa Kapaya(kulia) zenye makubaliano juu ya Mpango wa
Kuwarejesha Wakimbizi wa Burundi wanaohifadhiwa mkoani
Kigoma.Makubaliano hayo yamefanyika mwishoni mwa wiki, Ukumbi wa
Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere,jijini Dar es Salaam.Picha na
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Wakimbizi
wa Burundi waliokimbia machafuko nchini kwao wataanza kurejea nchini
kwao ifikapo Septemba 7 hadi Desemba 31, mwaka huu mara baada ya pande
tatu ikiwemo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Burundi na
Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR), kutiliana saini Mpango
wa Kuwarejesha wakimbizi baada ya mkutano uliochukua takribani siku tatu
katika kuandaa mpango huo.
Wakitiliana
saini makubaliano hayo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki,Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, Waziri wa Mambo ya Ndani na Elimu ya
Uzalendo kutoka nchini Burundi, Pascal Barandagiye na Mwakilishi wa
Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) nchini Tanzania, Chansa
Kapaya, mwishoni mwa wiki wote walikubaliana kutekeleza vipengele
vilivyopo katika makubaliano hayo yakiwa na lengo la kuwarudisha
wakimbizi walioomba kurejea nchini Burundi, baada ya hali ya Amani na
utulivu kurejea.
Akizungumza
baada ya kutiliana saini makubaliano hayo Waziri Mwigulu, alisema
umefika wakati wa wakimbizi wa Burundi kurudi nchini kwao kuungana na
familia zao na ndugu waliobaki ili kusaidia kujenga uchumi wa nchi yao
baada ya kuwa katika machafuko yaliyosababisha kukimbia nchi yao kwa
muda mrefu.
“Mimi
kama mwanauchumi ninaona madai yao ya kurudi nchini Burundi
kujishughulisha na shughuli za kilimo ni maamuzi mazuri huku pia
wakisisitiza kurejea kwa Amani na Utulivu nchini kwao kuwa ni sababu ya
msingi ya kufikia kuomba kurejea, sisi kama Serikali tutahakikisha zoezi
hilo la urejeaji nchini kwao linaenda salama tukishirikiana na Serikali
ya Burundi kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchini Burundi,” alisema
Mwigulu.
Naye
Waziri wa Mambo ya Ndani na Elimu ya Uzalendo kutoka nchini Burundi,
Pascal Barandagiye, amesema anaishukuru Serikali ya Tanzania na
Watanzania wanaoishi kwenye maeneo yaliyotumika kuwahifadhi wakimbizi
kwa ukarimu wao walioonyesha muda wote kwa raia kutoka nchini Burundi
huku akisisitiza kurejea kwa hali ya Amani na utulivu ambao hapo
mwanzoni ilitoweka.
“Nawaomba
wananchi wetu warejee nchini ili tuweze kuijenga Burundi yetu ambayo
hivi sasa kuna Amani na utulivu, pia naishukuru Serikali ya Tanzania na
Watanzania ambao wamekua wakiwaonyesha ukarimu wakimbizi kutoka Burundi
na kuwapa hifadhi nchini hapa,”alisema Barandagiye.

No comments:
Post a Comment