Msanii
wa muziki aliyewahi kufanya vizuri na wimbo Malavidavi, Mpenzi Jini na
nyingine nyingi, Z Anto, amefunguka kwa kusema kuwa wiki hii ataachia
kazi yake mpya huku akidai haamini kama kazi yake hiyo itashindwa
kufanya vizuri kwa kuwa Diamond na Alikiba wameachia kazi zao mpya
ambazo zinashindanishwa mitandaoni.
Akiongea
na waandishi wa habari Jumamosi hii jijini Dar es salaam, Z Anto amedai
yeye atapita katikati ya Diamond na Alikiba kwa kuwa muziki wake
unapendwa na watu wa rika zote na pia hauna makundi kama ulivyo wa
wawili wao.
"Wote
nawaweza sana, muziki wangu ni mtamu na hauna makundi kwahiyo kila mtu
anaweza kuusikiliza hata hao bila shaka ni mashabiki wa muziki wangu
ndio maana nikasema kuogopa kuachia ngoma sasa hivi kwaajili ya Diamond
na Alikiba utakuwa ni ujinga," alisema Z Anto.
Aliongeza
"Binafsi najiamini sana kwa sababu muziki wangu ni mzuri na tayari kuna
platfom ambayo niliiweka toka kipindi cha nyumba sema tu ukimya wangu
ndio umewapa nafasi hawa ndugu zangu lakini sioni kama nitatizo
kwasababu bado nafasi yangu naiona,"
Muimbaji
huyo amesema anajua muziki umebadilika sana ndio maana na yeye
amejipanga kuvingine ili kukabiliana na watu ambao wanashindana kwa sasa
kwenye muziki.
"Kila
mtu anatakua kuwa juu zaidi ya mwenzake na ukimya wangu umewapa nafasi
wasanii wengi sana na lengo langu ni kufanya vizuri zaidi ndio maana
nikasema sishindani na Diamond wala Alikiba mimi nitapita katikati yao
na mashabiki ndio wenye maamuzi ya mwisho katika hili kwahiyo mimi
ningesema tusubiri kazi mpya waisapport halafu ndio tuanze kupima,"
alisema Z Anto.
"Mimi
naamini msanii yoyete anaweza kufanya vizuri zaidi ya hata wakongwe kama
akijipanga vizuri muziki una sifa hiyo, kwahiyo mimi naweza kusema
lolote linaweza kutokea kwenye muziki lisiwe leo au kesho muda ukifika
hauwezi kushindana nao, wakati ni ukuta," alifafanua zaidi.
Katika
ujio wake muimbaji huyo amesema tayari ameandaa audio na video ambayo
itaanza kutoka na kuleta picha mpya katika muziki wake.
"Kazi
zipo tayari kwa sababu ni nyingi na naanza na moja moja, siku yoyote
kuanzia leo nitaachia kazi moja na baada ya upepo wa hapo nitaendelea
kasi hiyo hiyo kadri mambo yanavyokwenda," alisema Z.
No comments:
Post a Comment