HUU NDIYO UWANJA WA MPECHI AMBAO UNATUMIKA KWAAJILI YA KUZINDULIA MAADHIMISHO YA WIKI YA UHAMASISHAJI WA UNYWAJI MAZIWA KITAIFA AMBAPO MAANDALIZI YAMEKWISHA KAMILIKA.
MABANDA YA WAFUGAJI YAKIWA TAYARI YAMEKWISHA KAMILIKA KUJENGWA TAYARI KWA MAONESHO KESHO
NA MICHAEL NGILANGWA -NJOMBE
Kutoa Kipaumbele Cha Rishe Bora Kwa Watoto Wenye Umri Wa Chini Ya Miaka Mitano Ili Kuepukana Na
Matatizo Ya Ugonjwa Wa Utapiamro Ambao Idadi Ya Watoto Wenye Umri Huo Imezidi Kuongezeka Kwa
Zaidi Ya Asilimia 30 Kwa Mikoa Ya Kusini Wanaugua.
Rai Hiyo Imetolewa Na Mwenyekiti Wa Bodi Ya Maziwa Nchini Bi.Aichi Kitalyi Wakati Akizungumza Na
Uplands Fm Kuhusiana Na Uzinduzi Wa Wiki Ya Uhamasishaji Wa Unywaji Maziwa Ambao Umeonesha
Kiwango Cha Wananchi Na Watoto Wao Wanaokunywa Maziwa Kuwa Kidogo Licha Ya Mikoa Ya Nyanda
Za Juu Kusini Kuongoza Kwa Uzarishaji Wa Maziwa Nchini.
Bi.Kitalyi Amesema Viongozi Wa Halmashauri Na Mikoa Wanapaswa Kuongeza Juhudi Ya Kuwaelimisha
Wananchi Kutambua Umuhimu Wa Kunywa Maziwa Kwa Wingi Ili Kuongeza Afya Na Kupunguza
Kiwango Cha Ugonjwa Wa Utapiamlo Kwa Watoto Chini Ya Miaka Mitano Kwa Mikoa Ya Kusini Huku
Akisema Maziwa Yanamfanya Mtoto Kuwa Na Afya Bora Na Akili Darasani.
Kwa Upande Wake Msajili Wa Bodi Ya Maziwa Tanzania Nelson Kilongozi Amesema Maadhimisho Hayo
Ya 19 Yanatoa Fursa Kwa Wananchi Kuwa Na Tabia Ya Kunywa Maziwa Kila Siku Ili Kujenga Afya Zao
Ambapo Mtu Mmoja Anapaswa Kunywa Lita 200 Za Maziwa Kwa Mwaka Licha Yakuwa Baadhi Yao
Hawajatambua Umuhimu Wake Kwani Wanakunywa Lita 47 Tu Kwa Mwaka.
Akizungumzia Maandalizi Ya Uzinduzi Wa Maadhimisho Ya Unywaji Wa Maziwa Kitaifa Mwenyekiti Wa
Kamati Ya Maandalizi Ya Maadhimisho Hayo Daktari Wa Mifugo Mkoani Hapa Geoge Charles Katemba
Amesema Maandalizi Ya Uzinduzi Huo Yamekamilika Ambapo Mgeni Rasmi Anatarajiwa Kuwa Mkuu Wa
Mkoa Wa Njombe Dkt Rehema Nchimbi Huku Akitoa Ratiba Ya Maandamano .
Dkt Katemba Amesema Mkoa Wa Njombe Unang'ombe Zaidi Ya Elfu 15 Wa Maziwa Na Kusema Kuwa
Wafugaji Wamepokea Vizuri Elimu Ya Ufugaji Huo Ambapo Kwa Kipindi Cha Miaka 10 Iliyopita Mkoa Wa
Njombe Ulikuwa Na Ng'ombe Zaidi Ya Elfu 1500 Huku Uzarishaji Wa Maziwa Nao Ukiongezeka Na Kufikia
Zaidi Ya Lita Milioni 8 Kwa Mwaka Na Lita Elfu 24 Kwa Siku Zikizarishwa Ikiwa Kiwanda Kinauwezo Wa
Kuchukua Maziwa Lita 3500 Hadi 4500 Kwa Siku.
Kauli Mbiu Ya Maadhimisho Ya Uhamasishaji Wa Unywaji Wa Maziwa Kitaifa Inasema Jenga Tabia Ya
Kunywa Maziwa Kwa Afya Na Uchumi.
No comments:
Post a Comment