MWENYEKITI WA SERIKALI YA MTAA WA KIBENA WINFRED KAYOMBO AKIONESHA MBAO ZILIZOTOLEWA NA KAMPUNI HIYO
MWENYEKITI WA SERIKALI YA MTAA WA KIBENA HOSPITALI WINFRED KAYOMBO AKIWA MTAANI KWAKE KIBENA
MWENYEKITI WA SERIKALI YA MTAA HUO AMBAYE AMESEMA MBAO WALIZOPEWA NI KWAAJILI YA UJENZI WA OFISI YA MTAA INAYOJENGWA AMBAYO IMEFIKIA HATUA YA RENTA
MJUMBE WA SERIKALI YA MTAA WA KIBENA HOSPITALI BWANA MKISI AKIWA AMEFRAHI KWA KUPEWA MBAO
MWENYEKITI WA SERIKALI YA MTAA WA KIBENA HOSPITALI WA UPANDE WA KUSHOTO MWENYE KOTI JEUSI NA MWENYE KOFIA NI MJUMBE WA SERIKALI BWANA MKISI
PIA WAMEZUNGUMZIA CHANGAMOTO ZINAZOIKABILI SHULE YA MSINGI UJAMAA
Serikali Ya Mtaa Wa Kibena Hospitali Imekili Kuwepo Kwa Changamoto Mbalimbali Zinazoikabili Shule Ya Msingi Ujamaa Za Ujenzi Wa Nyumba Za Walimu Pamoja Na Vyoo Vya Wanafunzi Ambapo Tatizo Hilo Limedaiwa Kuendelea Kutatuliwa Taratibu Na Wananchi Wa Mtaa Wa Kibena Huku Wadau Na Halmashauri Zikiombwa Kusaidia Kumaliza Baadhi Ya Changamoto Zilizopo.
Akizunguma Na Mwenyekiti Wa Serikali Ya Mtaa Wa Kibena Hospitali Winfred Kayombo Amekili Kuwepo Kwa Changamoto Hizo Katika Shule Ya Msingi Ujamaa Na Kusema Serikali Ya Mtaa Huo Kwa Kushirikiana Na Wananchi Wa Mtaa Wamefanikiwa Kukamilisha Zoezi La Kusogeza Miundombinu Ya Maji Kwenye Shule Hiyo Kama Kipaumbele Chao Katika Elimu.
Aidha Bwana Kayombo Amesema Shule Hiyo Inakabiliwa Pia Na Changamoto Ya Uchakavu Wa Vyumba Vya Madarasa Ambapo Kwa Upande Wa Vyoo Wameanza Kukarabati Vilivyopo Wakati Serikali Ya Mtaa Huo Na Wananchi Wakijiandaa Kuanza Ujenzi Wa Vyoo Vya Kisasa Na Nyumba Za Walimu Ambapo Ameomba Halmashauri Nayo Kusaidia Kutatua Baadhi Ya Changamoto Zilizopo Kwenye Shule Hiyo.
Bwana Kayombo Amesema Kwa Kipindi Hiki Serikali Ya Mtaa Ipo Kukamilisha Ujenzi Wa Jengo La Ofisi Ambalo Limefikia Hatua Ya Renta Linalojengwa Kwa Nguvu Za Michango Ya Wananchi Huku Akipongeza Hatua Ya Kampuni Ya Tanwat Mjini Njombe Kwa Kuwasaidia Mbao Mia Nne Tisini Ambazo Tayari Wamekwisha Zichukua Kwaajili Ya Kukamilishia Ujenzi Wa Ofisi Hiyo.
Akizungumza Siku Chache Zimepita Kwenye Mkutano Wa Uzinduzi Na Kukabidhiwa Kisima Cha Maji Na Kampuni Ya Tanwat Mwalimu Mkuu Wa Shule Ya Msingi Ujamaa Cairo Ngakonda Alitaka Wananchi Na Serikali Kutoa Kipaumbele Kuboresha Miundombinu Ya Shule Kwa Kujenga Nyumba Za Walimu,Ukarabati Wa Vyumba Vya Madarasa Na Michango Mingine Ya Shule Ili Kuinua Kiwango Cha Taalumu Shuleni Hapo.
No comments:
Post a Comment