ERASTO MPETE AKIWA NA BANDA LAKE KATIKA UWANJA WA MPECHI SEKONDARI
GARI LA MAZIWA YA ASAS NAYO YASHIRIKI MAONESHO YA MAADHIMSHO YA UHAMASISHAJI WA UNYWAJI MAZIWA NJOMBE
SHIRIKA LA VIWANGO TANZANIA TBS HALIKUWA NYUMA KWENYE MAONESHO HAYO
WANAFUNZI WA SHULE MBALIMBALI ZA MJI WA NJOMBE ILIZOSHIRIKI UZINDUZI WA WIKI YA UHAMASISHAJI WA UNYWAJI MAZIWA MKOA WA NJOMBE
MAAFISA MASOKO WA SHIRIKA LA MAZIWA MKOA WA IRINGA NA NJOMBE ASAS
MSAJILI WA BODI YA MAZIWA TANZANIA NELSON KILANGOZI AKIWA KWENYE JUKWAA NA MGENI RASMI
MWENYEKITI WA BODI YA MAZIWA TANZANIA AICHI KITALYI AKIWAKARIBISHA WAGENI KABLA YA HOTUBA YA MGENI RASMI
KAIMU MWENYEKITI WA BARAZA LA MAZIWA TANZANIA MARK TSOXO AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI HUO
MGENI RASMI KWENYE UZINDUZI HUO KAIMU MKUU WA MKOA WA NJOMBE AMBAYE NI MKUU WA MKOA WA NJOMBE ANATORY CHOYA AKITOA HOTUBA YAKE KWENYE UWANJA VYA SHULE YA SEKONDARI MPECHI LEO
WANAFUNZI WA SHULE MBALIMBALI NA WASIYO WA SHULE WAKIFRAHIA KUNYWA MAZIWA
MWENYEKITI WA BODI YA MAZIWA TANZANIA AICHI KITALYI
MWAKILISHI KUTOKA WIZARANI
NA MICHAEL NGILANGWA-NJOMBE
Kaimu Mkuu Wa Mkoa Wa Njombe Anatory Choya Amewaagiza Walimu Wa Kuu Na Wakurugenzi Kuanzisha Utaratibu Wa Kufuga Ng'ombe Wa Maziwa Kwa Shule Za Sekondari Na Msingi Ili Wanafunzi Waweze Kunufaika Na Elimu Ya Ufugaji Wa Ng'ombe Hao Na Kutambua Umuhimu Wa Kunywa Maziwa Na Kuendelea Utalaamu Wa Kufuga Hata Wakirudi Uraiani.
Kauli Hiyo Na Kaimu Mkuu Wa Mkoa Huyo Choya Wakati Akiwa Mgeni Rasmi Kwenye Uzinduzi Wa Wiki Ya Uhamasishaji Wa Unywaji Maziwa Ambayo Kilele Chake Kinatarajia Kufanyika June Mosi Mwaka Huu Yakifanyikia Katika Uwanja Wa Shule Ya Sekondari Mpechi Mjini Njombe Ambapo Endapo Shule Zitakuwa Na Ng'ombe Mmoja Itasaidia Wanafunzi Kupata Maziwa Na Kujifunza Namna Wanavyoweza Kufuga.
Choya Amesema Wakurugenzi Wanatakiwa Kwenda Kufanya Kila Liwezekanalo Kwaajili Ya Kuhakikisha Shule Hizo Zinakuwa Na Ng'ombe Hao Na Kupeleka Watalaamu Wa Mifugo Ambao Watasimamia Na Kuelimisha Wanafunzi Namna Ya Kuwafuga Ng'ombe Hao Huku Akitaka Wazazi Kuhakikisha Wanapunguza Tatizo La Udumavu Kwa Watoto Kwa Kuwapatia Maziwa Kama Rishe Bora Kwa Watoto.
Katika Hatua Nyingine Choya Amewataka Wafanyabiashara Wa Maziwa Kuacha Tabia Ya Kuuza Maziwa Yaliyokwisha Muda Wake Wa Matumizi Kwa Binadamu Kwani Siku Chache Zilizopita Kuna Baadhi Ya Wafanyabiashara Wamekamatwa Wakiwa Na Maziwa Yaliyokwisha Muda Wake Jambo Ambalo Linasababisha Wananchi Kupata Madhara Ya Magonjwa Bila Kujitambua.
Awali Akizungumza Mwenyekiti Wa Bodi Ya Maziwa Tanzania Daktari Wa Mifugo Aichi Kitalyi Pamoja Na Kupongeza Wananchi Wa Mkoa Wa Njombe Kwa Juhudi Za Kuzarisha Na Kuendeleza Mpango Wa Unywaji Maziwa Lakini Amesema Wananchi Wanatakiwa Kunywa Maziwa Kama Chakula Na Siyo Kama Dawa Na Elimu Itaenea Kwa Wananchi Wote Katika Kipindi Hiki ChaMaadhimisho Hayo.
Kwa Upande Wake Makamu Mwenyekiti Wa Baraza La Wadau Wa Maziwa Bwana Mark Tsoxo Amesema Mkoa Wa Njombe Una Hali Ya Hewa Nzuri Inayoruhusu Ustawishaji Wa Ng'ombe Wa Maziwa Na Hivyo Wadau Na Wananchi Wanatakiwa Kuwekeza Kwenye Ufugaji Wa Ng'ombe Wa Maziwa Huku Akiomba Serikali Kusaidia Kuweka Mazingira Mazuri Yanayovutia Uwekezaji Wa Maziwa Kwa Sekta Binafsi.
Kauli Mbiu Ya Maadhimisho Hayo Kwa Mwaka Huu Inasema Jenga Tabia Ya Kunywa Maziwa Kwa Afya Na Uchumi.
No comments:
Post a Comment