Mohamed
Taqi Khan (20) raia wa Jamhuri ya Watu wa Iran akionyesha uwezo na
kipaji chake cha kuhifadhi Quraan tukufu katika uwanja wa shule ya
Msingi Mbugani katika Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza.Ana uwezo wa
kutumia njia 52 kuelezea Quraan.Waliomshikia vinasa sauti (Microphone)
kulia ni Sheikh Ramadhan Hashimu na kushoto ni Mohamed Naqi Taqi.
Mohamed
Naqi Khan (20) akionyesha kipaji na uwezo wake wa kuelezea Quraan
ambayo ameihifadhi kichwani akiwa na umri wa miaka 10, miaka saba baada
ya wazazi wake kufariki dunia na antumia njia 52 kuelezea Quraan hiyo.
Hapa akionyesha kipaji chake hicho kwenye uwanja wa Shule ya Msingi
Mbugani Jijini Mwanza na kutokana na kipaji chake hicho amekuwa kivutio
kwa maelfu ya waumini wa dini ya Kiislamu akiwa ameendesha vipindi zaidi
2000 katika nchi za Kiislamu katika miji mbalimbali.
KATIBU
wa Bakwata wa Mkoa wa Mwanza Mohamed Salum Balla akizungumza baada ya
dua maalumu ya kuwaombea waumini wa dini ya kiislamu waliouawa wakiswali
katika msikiti wa R Rahman Ibanda Relini.Dua hiyo ilisomwa katika
Uwanja wa shule ya Msingi Mbugani jijini Mwanza juzi na kuhudhuriwa na
Sheikh Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Alhaji Salum Ferej wa pili kulia kwa
Balla wa pili ni Sheikh Hassan Kabeke ambaye ni Mwenyekiti mwenza wa
Amani na wa pili kutoka kulia ni Mwenyekiti wa wa Bodi ya wadhamini ya
TIC Dk. Mohamed Kanju .
Katibu

TIC Dk. Mohamed Kanju ,Alhaji Sibtain Meghjee ambaye ni Mwenyekiti wa
Taasisi ya Bilal Muslim Mission of Tanzania, wa kwanza kulia.
Picha zote na Baltazar Mashaka
No comments:
Post a Comment