Manufaa yanayotokana na hifadhi za taifa na vivutio vya utalii
hayatoshi tu kutumika kama nyenzo ya kupunguza vitendo vya ujangili na
uvamizi katika maeneo yaliyotengwa na serikali ikiwa hakutakuwa na
ushirikishwaji wa kutosha na wa moja kwa moja kwa wananchi wanaoishi
maeneo yanayozunguka rasilimali hizo.
Pamoja na mchango mkubwa wa utalii katika uchumi taifa na kuwepo
kwa manufaa kwa vijiji vinavyozunguka hifadhi za taifa na vitutio
vingine vya utalii, jamii bado imeshindwa kuzitambua faida hizo ili
kushiriki kikamilifu katika kupambana na ujangili na uvamizi holela wa
maeneo hayo.
Je, jitihada zinazofanywa na serikali na wadau kutoa elimu kwa jamii na kuibua fursa muhimu katika sekta hii zinatosha?
Ili kujibu swali hilo Jukwaa linalohusu masuala ya Usimamizi
Shirikishi wa jamii wa maliasili mnamo Mei 26, 2016 limewakutanisha
wadau wa mazingira, maliasili na utalii kujadili mambo muhimu yanayoweza
kuchangia katika kufungua milango ya fursa katika sekta ya
wanayamapori.
Mratibu wa Jumuiko la Maliasi Tanzania (TNRM), Faustine Ninga
akifafanua jambo wakati wa Jukwaa la Masuala ya Usimamizi Shirikishi wa
Jamii wa Maliasili lililofanyika Mei 26, 2016 jijini Dar es Salaam.
Demetrius Kweka kutoka Engility, (wasimamizi na waendeshaji wa
mradi wa PROTECT), akizungumzia hatua mbalimbali za utekelezaji wa mradi
huo
Wadau wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa mkutano huo
Afisa Utalii Mwandamizi kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Wilfred Msemo akiwasilisha mada
Meneja Msaidizi wa Hifadhi ya Taifa ya Selous, akiwasilisha mada
wakati wa Jukwaa la Masuala ya Usimamizi Shirikishi wa Jamii wa
Maliasili lililofanyika Mei 26, 2016 jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment