Thursday, May 26, 2016
JESHI LA LA POLISI LINAMSHIKILIA MWALIMU KURWA NELSON WA SHULE YA MSINGI IWAFI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MWANAFUNZI WA MIAKA 12
KAIMU KAMANDA WA JESHI LA POLISI MKOA WA NJOMBE JOHN CHARLES TEMU AKITOA TAARIFA YA KUBAKWA KWA MWANAFUNZI MWENYE UMRI WA MIAKA 12.
Jeshi La Polisi Mkoa Wa Njombe Linamshikilia Mwalimu Kurwa Nelson Wa Shule Ya Msingi Iwafi Kata Ya Idamba Kwa Tuhuma Ya Kuwa Na Mahusiano Ya Kimapenzi Na Mwanafunzi Mwenye Umri Wa Miaka 12 Anayesoma Darasa La Sita Katika Shule Hiyo Kinyume Na Maadili Ya Kiutumishi Ambapo Uchunguzi Ukikamilika Anatarajiwa Kufikishwa Mahakamani Wakati Wowote.
Kaimu Kamanda Wa Jeshi La Polisi Mkoa Wa Njombe John Charles Temu Amethibitisha Kushikiliwa Kwa Mwalimu Kurwa Nelson Wa Shule Ya Msingi Iwafi Wilayani Njombe Ambapo Mtuhumiwa Huyo Amekamatwa Mnamo Mei 21 Kwa Tuhuma Za Kuwa Na Mahusiano Ya Kimapenzi Na Mwanafunzi Wake Kwa Kipindi Tofauti.
Diwani wa Kata ya Idamba Wilayani Njombe Melkizedeki Kabelege Amekili Kupata Taarifa Ya Mwalimu Huyo Kushikiliwa Kwa Tuhuma Za Kuwa Na Mahusiano Ya Kimapenzi Na Mwanafunzi Wake Licha Yakusema Hajapata Taarifa Rasmi Kutoka Kwa Viongozi Wa Kijiji Hicho Na Kulazimika Kuwaagiza Maafisa Watendaji wa Kata ya Idamba na Kijiji cha Iwafi Kufuatilia Tukio Hilo Kisha Kutoa Taarifa Katika Ofisi Yake.
Diwani Kabelege Ametoa Maagizo Kwa Watendaji Hao wa Kata na Kijiji Kufuatia Taarifa Zinazozagaa Katika Kijiji cha Iwafi Juu ya Tuhuma za Mwalimu Kumbaka Mwanafunzi Huku Viongozi Wa Serikali Ya Kijiji Wakishindwa Kutoa Taarifa Za Mwalimu Huyo Anayeshikiliwa Na Jeshi La Polisi Wilaya Ya Njombe Tangu Mei 21 . .
Aidha Diwani Huyo Ameonesha Kusikitishwa Kwake na Viongozi wa Vijiji Kwa Kushindwa Kuonesha Ushirikiano Juu ya Matukio Yanayojitokeza Huku Akiwaomba Wananchi Kushirikiana na Vyombo Vya Sheria Katika Kupambana na Vitendo Vya Unyanyasaji , Ukatili Pamoja na Uhalifu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment