MOTO UNAOTEKETEZA BIDHAA ZILIZOKWISHA MUDA WAKE KWA WAFANYABIASHARA NJOMBE
KAIM MKUU WA MKOA WA NJOMBE ANATORY CHOYA AMBAYE NI MKUU WA WILAYA YA LUDEWA AKIWASHA MOTO KWAAJILI YA KUTEKETEZA BIDHAA HIZO
HIZI NDIZO BIDHAA ZILIZOKAMATWA ZIKIUZWA KWENYE MADUKA YA WAFANYABIASHARA MKOA WA NJOMBE ZIKIWA ZIMEKWISHA MUDA WAKE BAADA YA MSAKO MKALI WA SIKU MBILI
MENEJA WA MAMLAKA YA CHAKULA ,DAWA NA VIPODOZI KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI KWA MIKOA YA MBEYA,IRINGA,NJOMBE ,KATAVI NA SONGWE RODNEY ALANANGA AKITOA TAARIFA FUPI MBELE YA KAIM MKUU WA MKOA WA NJOMBE KABLA YA KUTEKETEZA BIDHAA HIZO
HUYU NI KAIMU MKUU WA MKOA WA NJOMBE AMBAYE NI MKUU WA WILAYA YA LUDEWA ANATORY CHOYA AKIZUNGUMZA KABLA YA KUTEKETEZA BIDHAA HIZO
KAIM MGANGA MKUU WA MKOA WA NJOMBE GABRIEL NGOBEKO AKISHUHUDIA ZOEZI HILO LA UTEKETEZAJI WA BIDHAA HIZO KWENYE DAMPO LA MAHEVE MJINI NJOMBE
KAIMU MKUU WA MKOA WA NJOMBE AMBAYE NI MKUU WA WILAYA YA LUDEWA ANATORY CHOYA AKIWASHA MOTO WA KUCHOMEA BIDHAA ZILIZOKWISHA MUDA WAKE
KAIMU MKUU WA MKOA WA NJOMBE AMBAYE NI MKUU WA WILAYA YA NJOMBE ANATORY CHOYA AKIWA NA MENEJA WA TFDA KANDA RODNEY ALANANGA WAKITOKA KUELEKEA KWENYE MAGARI YAO BAADA YA KUTEKETEZA BIDHAA ZILIZOKAMATWA MKOA WA NJOMBE ZIKIWA ZIMEKWISHI MUDA WAKE.
NJOMBE
Mamlaka Ya Chakula ,Dawa Na Vipodozi Kanda Ya Nyanda Za Juu Kusini Jana Imeteketeza Kilo 1000 Za
Bidhaa Zilizokwisha Muda wa Matumizi Kwa Binadamu Zenye Thamani ya Zaidi Ya Shilingi Milioni Kumi
Ambazo Zimekamatwa Katika Halmashauri Ya Mji Na Wilaya Ya Njombe Kufuatia Msako Ulioendeshwa Na
Mamlaka Hiyo Kwa Muda Wa Siku Mbili.
Akiteketeza Bidhaa Hizo Kaimu Mkuu Wa Mkoa Wa Njombe Anatory Choya Amewatahadharisha Wananchi
Na Wafanyabiashara Mkoa Wa Njombe Kuwa Makini Na Bidhaa Zilizopitwa Muda Wake Wa Matumizi
Kwa Binadamu Huku Akikemea Baadhi Ya Wafanyabiashara Wanaouza Bidhaa Ambazo Muda Wake Wa
Matumizi Umekwisha Kwani Wanahatarisha Afya Za Watumiaji.
Aidha Kaimu Mkuu Wa Mkoa Huyo Choya Ametaka Msako Kuendelea Kufanyika Kwenye Maduka
Mbalimbali Ya Biashara Ili Kutokomeza Tabia Ya Baadhi Ya Wafanyabiashara Wanaoingiza Na Kuuza
Biadhaa Zilizopigwa Marufuku Na Serikali Huku Akiitaka Mamlaka Ya Chakula Na Dawa Kuwafutia Leseni
Za Biashara Wanaobainika Wakiziingiza Na Kuuza Biadhaa Zilizopitwa Na Muda Wake Wa Matumizi.
''Niwatahadharishe sana wananchi na wafanyabiashara wote wa Mkoa wa njombe kitendo cha kuendelea
kuuza bidhaa hizi ambazo zimepitwa na wakati ni kuwaumiza watumiaji hivyo wafanyabiashara mnatakiwa
kuacha tabia ya kuuza bidhaa zilizokwisha muda wake kwa kuwa makini na biadhaa hizo''Alisema kaim
mkuu huyo wa mkoa.
Choya amesema wafanyabiashara walio wengi bidhaa zilizokwisha muda wake na zinazohatarisha usalaama
wa afya za wananchi wao hawatumii bidhaa hizo danganyifu isipokuwa wao wanaangalia faida na siyo kujali
afya za watumiaji na kwamba kitendo hicho ni cha kumkufuru Mungu na wawe wazalendo
''Nasema tena nasema baadhi ya wafanyabiashara hawatumii wao bidhaa zilizokwisha muda wake isipokuwa
wanauza ilimradi wapate faidi lakini kiyama kinawaijia kiyama kinawaijia wajuwe kwamba Serikali
inamacho kama chandarua tumeshawafahamu tumeshawabaini na ifika mahala TFDA chukueni hatua kali
ikiwa ni pamoja na kuwanyang'anya leseni zao kwa sababu amekwisha bainika kuwa siyo mwaminifu''
Alisema kaimu mkuu wa mkoa Anatory Choya.
Kaimu mkuu huyo wa mkoa ambaye ni mkuu wa Wilaya ya Ludewa Anatory Choya ameshauri Mamlaka ya
chakula,dawa na vipodozi kufungua ofisi zao kwa kila mkoa na kujiwekea utaratibu wa kupitia mara kwa
mara kwenye maduka ya biashara kuliko kutokea Mbeya ambako ni makao makuu ya kanda wananchi
wanaangamizwa usalaama wa afya zao kwani wakikaa muda mrefu wafanyabiashara wanajisahau.
''Mukiwabaini wafanyabiashara wanaokiuka kanuni na sheria wapeni taarifa mamlaka zote zinazohusika
zikiwemo usalaama wa Taifa,Jeshi la polisi,Mkuu wa mkoa apewe taarifa,Uhamiaji wapewe taarifa
,Takukuru na viongozi wengine wa mahali mlipo kwa viongozi wapewe taarifa ili kutokomeza tabia kama
hiyo ya kuuza bidhaa zilizokwisha muda wake zipunguwe au kumaliza kabisa''Alisema Choya .
Akitolea Taarifa Fupi Ya Upatikanaji Wa Bidhaa Zilizopitwa Na Muda Wa Matumizi Kwa Minadamu Mkoa
Wa Njombe Meneja Wa Mamlaka Ya Chakula, Dawa Na Vipodozi Kanda Ya Nyanda Za Juu Kusini TFDA
Rodney Alananga Amesema Wamefanikiwa Kukamata Watu 57 Wa Halmashauri Ya Mji Na Wilaya Ya
Njombe Na Kufanikiwa Kukamata Bidhaa Mbalimbali Zilizopitwa Muda Wake
Bwana Alananga Amesema Katika Msako Huo Wamefanikiwa Kukamata Bidhaa Zinauzwa Zikiwa
Zimekwisha Muda Wake Wa Matumizi Zikiwemo Red Bu,Majani Ya Chai,Pipi Za Watoto Ambazo
Zinaendelea Kuuzwa Zikiwa Zimekwisha Muda Wake, Bidhaa Ambazo Hazijaruhusiwa Kuingia Kihalali
Kutumika Nchini,Maziwa Ya Watoto Yasiyo Sajiliwa, Pombe Kali Viroba Kutoka Nchi Jirani,Vipodozi Na
Ponmpas.
''Bidhaa Hizi ni hatari kwa matumizi ya binadamu kwani bidhaa hizo zina sumu ambayo ni hatari kwa
watumiaji nawaomba wananchi kujenga mazoea ya kusoma mwisho wa tarehe ya bidhaa ambazo
wananunua ili kulinda afya zao''.
Alananga amesema wafanyabiashara wanatakiwa kuzingatia sheria na uingizaji wa bidhaa wanazouza na ni
vizuri kununua bidhaa kwenye vyanzo maalumu na kudai lisiti ili kuisadia mamlaka hiyo kuwabaini
wanaouza bidhaa zilizokwisha muda wake.
Akizungumza Mara Baada Ya Kuteketeza Biadhaa Zilizokwisha Muda Wa Matumizi Mratibu Wa TFDA
Mkoa Wa Njombe Innocensia Mtega Amesema Mamlaka Hiyo Imekuwa Ikipita Mara Kwa Mara Kwa
Wafanyabiashara Wa Mkoa Wa Njombe Kutoa Elimu Ya Kuvitambua Vyakula ,Dawa Na Vipodozi
Vilivyokwisha Muda Wake Na Kutambua Tatizo Kuwepo Kwa Wafanyabiashara Wanaouza Bidhaa Za Jumla
Kuzihifadhi Na Kuwauzia Wafanyabiashara Wa Vijijini.
No comments:
Post a Comment