Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na wafanyabiashara
katika soko la machinga Complex leo mara baada ya kutembelea na Kamati
ya Ulinzi na Usalama jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar eS Salaam, Paul Makonda (mwenye tinted kushoto) akiwa na
Kamati ya Ulinzi na Usalama wakitembelea soko la machinga Complex leo
jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar eS Salaam, Paul Makonda (mwenye suti mbele) akiwa na
Kamati ya Ulinzi na Usalama wakitembelea soko la machinga Complex leo
jijini Dar es Salaam.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
SERIKALI
ya Mkoa wa Dar es Salaam imesema kuwa waliongia mkataba wa ujenzi wa
soko la Machinga Complex unatatizo kutokana fedha nyingi kudaiwa baada
ujenzi sh.bilioni 36 huku ujenzi wa jengo hilo ni zaidi ya sh.bilioni
12.
Akizungumza
leo baada ya kutembelea jengo hilo Mkuu wa Mkoa na Kamati ya Ulinzi na
Usalama wa Mkoa, Makonda amesema kuwa kutokana hali hiyo anaunda kamati
kuanzia kesho kuchambua mkataba huo kujua ni nani wamehusika na kwa nini
waliingia au waliingia wakiwa wamekunywa pombe.
Amesema
baada ya kuchambua wale waliohusika katika mazingira ya rushwa
watachukuliwa hatua kutokana na kuiongezea mzigo serikali kwa masilahi
yao.
Makonda
amesema hata utaratibu wa ugawaji wa vizimba una matatizo kutokana
baadhi ya watumishi wenye nafasi zao kumiliki vizimba na kupangisha
watu wafanyabiashara.
‘’Nitahakikisha
mkataba wa machinga Complex una majibu ya kutosha juu ni nani
waliohusika katika kubebesha mzigo serikali kwa wananchi wake’’ .amesema
Makonda
Amesema
katika mazingira hayo jengo hilo kwa fedha hiyo watu wafanyabiashara
hawawezi kuilipa mpaka kuangaliwa uhalali wa mkataba wa ujenzi wa jengo
hilo.
Aidha
amesema kuwa wananchi wa Dar es Salaam lazima wachukie rushwa ili kuweza
kupata huduma bora ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa za rushwa na
wanaotoa hata kama wanyonge hatua zitachukuliwa.
Amesema
katika wafanyabiashara ndogo ndogo wanaozungusha biashara zao katika
mitaa waombe maeneo ya kufanyia kazi na kuweza serikali kupata kodi
yake.
No comments:
Post a Comment