Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO
Halmashauri
ya Wilaya ya Lindi iliyopo Mkoa wa Lindi imetenga jumla ya shilingi
milioni 162 katika mwaka wa fedha 2016/17 kwa ajili ya kuisaidia shule
ya Msingi Nyangao.
Hayo
yamesemwa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Bi. Olliver
Vavunge alipokuwa akikanusha kuhusu madai ya wazazi kutaka shule hiyo
ifungwe kwa sababu ya ukosefu wa huduma muhimu.
“Kwa
kuwa shule hiyo tayari ina mabweni pamoja na bwalo la chakula, katika
bajeti iliyotengwa na Halmashauri kwa mwaka huu wa fedha jumla ya
shilingi milioni 100 zitatumika katika ujenzi wa uzio wa shule pamoja
na marekebisho madogo madogo ya shule hiyo na shilingi milioni 62
zitatumika kwa ajili ya chakula”alisema Bi. Olliver
Aidha,
Bi. Olliver amekanusha kupewa bajeti ya shilingi laki tisa kwa ajili
ya matumizi ya shule hiyo kwa mwezi kama ilivyoripotiwa kwenye baadhi ya
vyombo vya habari na kusema kuwa Serikali inatoa jumla ya shilingi
milioni 1.6 kwa kila mwezi.
Ameongeza
kukanusha kuwa si kweli kuwa wanafunzi wanakula mlo mmoja kwa siku bali
wanapata milo yote mitatu kama ilivyo kawaida.Shule ya Msingi Nyangao
ni shule ya watoto wenye mahitaji maalumu (walemavu) ambayo hadi sasa
ina jumla ya wanafunzi 42 na inahudumiwa na Serikali kwa mahitaji yote.
No comments:
Post a Comment