MKUU WA JESHI LA POLISI WILAYA YA NJOMBE OCD SSP MSOLO H.MSOLO AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI
Jeshi La Polisi Wilaya Ya Njombe Limewataka Wananchi Wanaomiliki Silaha Kujitokeza Kwa Wingi Kupeleka Silaha Zao Ili Zitambuliwe Kisheria Ambapo Watakaoshindwa Kupeleka Silaha Hizo Zihakikiwe Msako Utakapo Anza Watakaobainika Kumiliki Kinyume Na Maagizo Hayo Hatua Kali Zitachukuliwa Dhidi Yao.
Akizungumza Na Uplands Fm Mkuu Wa Jeshi La Polisi Wilaya Ya Njombe Msolo Hamisi Msolo Amesema Kuna Sheria Inayomuruhusu Mwananchi Kumiliki Silaha Kwa Kupitia Sehemu Mbalimbali Za Kamati Na Wakaguzi Ikiwemo Kupitishwa Na Baraza La Kata ,Kamati Ya Ulinzi Wilaya Na Kamati Ya Usalama Ya Mkoa Ambao Watathibitisha Uhalali Wa Kumiliki Silaha Yoyote.
OCD Msolo Amesema Katika Zoezi La Umiliki Wa Silaha Masharti Yake Ni Kwamba Yeyote Anayemiliki Silaha Kihalali Anatakiwa Apeleke Silaha Yeke Akiwa Na Kitabu Cha Umiliki Wa Silaha Yake,Awe Amelipia Karo Zake Zote Na Kwamba Baada Ya Zoezi La Uhakiki Kumalizika Kitabu Chake Atakachopewa Kiwe Kimeandikwa Silaha Yake Imesajiliwa Tarehe Ya Alipokwenda Kusajili Na Askali Aweke Namba Zake Aliyefanya Zoezi Hilo.
OCD Msola Amesema Zoezi La Msako Litaanza Kufanyika Baada Ya Mwezi June 30 Ikiwa Limeanza April Mosi Mwaka Huu Na Kwamba Sheria Ya Kumiliki Silaha Inazingatia Umri Na Sababu Ya Kutaka Kumiliki Silaha Nakusema Kuwa Sababu Moja Wapo Ni Kulinda Mali Zake Na Usalaama Wake Mwenyewe Binafsi .
Tayari Hadi Sasa Baadhi Ya Wananchi Wanaomiliki Silaha Wameanza Kujitokeza Kwenda Kuhakiki Silaha Zao Katika Ofisi Ya Ocd Wilaya Ya Njombe Ambapo Wito Unatolewa Kwa Wananchi Wote Wanaomiliki Silaha Zao Kujitokeza Kuhakiki Na Kusajili Kwa Mujibu Wa Sheria.
No comments:
Post a Comment