Wednesday, April 20, 2016
SAKATA LA MGOGORO WA MASHAMBA BAINA YA VIJIJI VYA MHAJI NA MAWINDI LASHINDWA KUFIKIA MWAFAKA
Siku Chache Baada Ya Kituo Hiki Kurusha Taarifa Za Sakata La Mgogoro Kati Ya Mhaji Na Mawindi ,Uongozi Wa Kata Ya Igima Wilayani Wanging'ombe Umesema Umeshindwa Kutatua Mgogoro Wa Mashamba Baina Ya Vijiji Hivyo Kutokana Na Tatizo Hilo Kuwa Ngazi Ya Wilaya, Tatizo Lililodaiwa Kuanza Tangu Mwaka 2014 Bila Kupatiwa Ufumbuzi Wowote Na Viongozi Waliokuwepo.
Kauli Hiyo Imetolewa Na Diwani Wa Kata Ya Igima Paulina Samata Mwinami Wakati Akizungumza Na Uplands Fm Kuhusiana Na Uhalali Wa Kijiji Cha Mhaji Kuzuia Mashamba Hayo Yasichukuliwe Na Kijiji Cha Mawindi Ambapo Amesema Mawindi Walijitenga Na Kijiji Hicho Hivyo Hakuna Sababu Ya Mawindi Kuchukua Mashamba Hayo Kutokana Na Mipaka Kuonesha Uharisia Wake .
Mwinami Amesema Kutokana Na Kijiji Cha Mawindi Kuomba Mashamba Kutoka Kijiji Cha Mhaji Kunakukubaliwa Ama KutoKubaliwa Huku Akiomba Wadau Wa Amani Kujitokeza Kutoa Ushauri Kumaliza Tatizo Hilo Ili Amani Iwepo Baina Ya Vijiji Hivyo Na Kusema Jitihada Za Kuomba Maeneo Kutoka Kampuni Ya Tanwat Kwaajili Ya Mawindi Zimeshafanyika Wanasubiria Majibu Ya Maombi Yao.
Wakizungumza Siku Chache Zilizopita Wananchi Wa Kijiji Cha Mawindi Wamesema Endapo Hawatafikia Mwafaka Wa Kupewa Mashamba Ekari Tisa Na Nusu Kutoka Mashamba Ya Kijiji Cha Mhaji Wako Tayari Kuvunja Kijiji Chao Na Kuwa Kijiji Kimoja Na Mhaji Na Kubainisha Kwamba Maombi Yao Ni Kupewa Fidia Wananchi Waliohamishwa Wakati Shule Ya Msingi Mawindi Ikijengwa.
Kwa Upande Wake Wananchi Wa Kijiji Cha Mhaji Pamoja Na Kumlaumu Mkuu Wa Wilaya Hiyo Kuliamuru Jeshi La Polisi Limshikiliye Mwenyekiti Wao Kwa Saa 24 Kwa Kosa La Kutopeleka Wananchi Wakati Akigawa Mashamba Na Kulazimisha Kugawa Maeneo Hayo ,Wamesema Hawako Tayari Kutoa Mashamba Hayo Kwani Mipaka Inaonesha Wazi Kati Ya Kijiji Cha Mawindi Na Mhaji.
Kwa Upande Wake Mkuu Wa Wilaya Ya Wanging'ombe Asunta Mshana Akizungumza Amesema Hawezi Kushinda Anatoa Maamuzi Ya Kijiji Kimoja Kwani Yeye Alikwisha Toa Maamuzi Yakwamba Vijiji Hivyo Vigawane Maeneo Hayo Nusu Kwa Nusu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment