HIZI NDIZO BARABARA ZA NJOMBE AMBAZO ZIMEPANDISHA NAULI KUTOKA SHILINGI ELFU KUMI HADI KUFIKIA ELFU 30 KWENDA TU.
Picha kwa Hisani ya Mtaa kwa Mtaa Blog
Rai Hiyo Imetolewa Na Wananchi Hao Wakati Wakizungumza Na Waandishi Wa Habari Kuhusiana Na Changamoto Ya Usafiri Inayowakabili Wananchi Wa Maeneo Hayo Na Kusema Kuwa Msimu Wa Mvua Imekuwa Kikwazo Kwa Magari Ya Abiria Na Mizigo Kuingia Mavanga Kwaajili Ya Kuchukua Abiria Na Mizigo Ya Kupeleka Njombe Na Madaba .
Aidha Wananchi Hao Pia Wamemuomba Mbunge Wa Wilaya Ya Rudewa Kufanya Mazungumza Na Mbunge Wa Madaba Na Kumaliza Tatizo La Uharibifu Wa Miundombinu Hiyo Ambapo Kuna Maeneo Korofi Ya Upande Wa Kata Ya Mavanga Wilaya Ya Ludewa Na Kuna Maeneo Yalioharibika Katika Wilaya Ya Madaba Barabara Ya Kutokea Mavanga.
Kufuatia Kuwepo Kwa Changamoto Hiyo Wananchi Hao Wamedai Kushindwa Kusafiri Na Kushinda Na Watoto Bila Kupata Huduma Yoyote Ya Chakula Na Wakati Mwingine Wanalazimika Kusafiri Usiku Kutokana Na Magari Kukwama, Na Ukosefu Wa Vyombo Vya Usafiri Hususani Msimu Wa Mvua Kutokana Na Wamiliki Wake Kugomea Kupeleka Magari Kwa Kuhofia Kuharibika.
Akizungumzia Changamoto Hiyo Diwani Wa Kata Ya Mavanga Emmanuel Ngalalekwa Amekili Kuwepo Kwa Changamoto Hiyo Ya Kukwama Magari Msimu Wa Mvua Na Kuwepo Kwa Usafiri Mchache Wa Magari Hali Inayosababisha Wasafiri Kutembea Usiku Kuanzia Saa Tisa Usiku Kwenda Kwenye Kituo Cha Basi Kuwahi Usafiri Ambapo Amesema Serikali Bado Inaendelea Na Jitihada Za Kuweka Kifusi Kuondoa Adha Hiyo.
No comments:
Post a Comment