Wednesday, April 20, 2016
SUMATRA NJOMBE YAJIPANGA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI MADEREVA WATAKAOKIUKA SHERIA NA BARABARANI
AFISA MFAWIDHI WA SUMATRA MKOA WA NJOMBE JOSEPH BURONGO AKIZUNGUMZA NA MADEREVA DARADARA NA BAJAJI
Mamlaka Ya Usafiri Wa Nchi Kavu Na Majini Nchini Sumatra Mkoa Wa Njombe Imewataka Viongozi Wa Usafirishaji Wa Vyombo Vya Moto Watokana Na Wamiliki Wa Vyombo Hivyo Ama Dereva Mwenye Mkataba Wa Ajira Na Mmiliki Wa Chombo Cha Moto Ambapo Kiongozi Yeyote Atakaye Kuwa Hana Vigezo Hivyo Hatapokelewa Na Mamlaka Hiyo.
Kauli Hiyo Imetolewa Na Afisa Mfawidhi Wa Sumatra Mkoa Wa Njombe Joseph Burongo Wakati Akizungumza Na Madereva Na Wamiliki Wa Magari Madogo Maarufu Kama Daradara Na Bajaji Kwamba Ofisi Ya Sumatra Haitawatambua Viongozi Wa Vyombo Hivyo Ambao Watakuwa Hawajakidhi Vigezo Vya Kuwa Mmiliki Ama Dereva Mwenye Mkataba Wa Ajira Na Bosi Wake.
Aidha Burongo Amesema Jeshi La Polisi Kupitia Kitengo Cha Usalaama Wa Barabarani Wanatakiwa Kuwaondoa Baadhi Ya Watu Wanaofanya Kazi Ya Usimamizi Wa Magari Hususani Wa Daradara Na Mawakala Ambao Wamekuwa Wakikamata Magari Kama Maafisa Usalaama Ikiwa Siyo Kazi Yao Huku Akiwataka Wenye Tabia Hiyo Kuacha Mara Moja Kwani Watachukuliwa Hatua Za Kisheria.
Katika Hatua Nyingine Afisa Sumatra Burongo Amesema Serikali Imeanzisha Mikakati Mipya Kwa Wanaokiuka Sheria Za Usalaama Barabarani Kwa Kupelekwa Mahakamani Kujibu Tuhuma Zitakazokuwa Zinawakabili Za Kuhusika Na Kosa Lolote La Usalama Wa Barabarani Ambapo Hadi Sasa Zoezi La Kuwafikisha Mahakamani Baadhi Ya Wanaokiuka Tayari Limeanza.
Burongo Amesema Ili Kuwabaini Wanaokiuka Sheria Na Kanuni Za Barabarani Sumatra Mkoa Wa Njombe Kwa Kushirikiana Na Jeshi La Polisi Itaanza Kufanya Oparation Ya Kuwabaini Wakiukaji Na Kuwapeleka Mahakamani Huku Akitaka Wamiliki Na Madereva Wa Vyombo Vya Moto Kuzingatia Masharti Waliopewa Na Maafisa Wa Usalaama Wa Barabarani Na Sumatra.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment