Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Inj. Gerson Lwenge, akiwa kwenye Mradi wa Kuzalisha na Kusambaza Majisafi wa Musoma Mjini ambao utekelekezaji wake utagharimu Sh. Bil 45 ambao unategemewa kukamilika Juni, 2016 na unategemewa kutoa huduma ya maji katika Manispaa ya Musoma kwa zaidi ya asilimia 90.
Mtambo
wa Kusafisha na Kutibu Maji ambao ni moja ya sehemu ya Mradi wa
Kuzalisha na Kusambaza Majisafi wa Musoma Mjini ambao utekelezaji wake
umefikia asilimia 75 kwa sasa.
Waziri
wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Inj. Gerson Lwenge akiweka jiwe la msingi
la ujenzi wa tanki la Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Musoma
(MUWASA) lenye mita za ujazo 135,000 eneo la Rwamlimi, Halmashauri ya
Manispaa ya Musoma ambalo linategemewa kuhudumia wakazi 1,000.
Mradi
wa Maji wa Lugeye-Kigangama, Magu, mkoani Mwanza ambao unatekelezwa
kupitia Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji ukiwa katika hatua za
ukamilishaji, ambao unatarajiwa kuhudumia wakazi wapatao 11,000
utagharimu zaidi ya Sh. bilioni 1.
- Sehemu ya Mradi wa Maji na Usafi wa Mazingira mjini Sengerema LV WATSAN II, eneo la Nyamazugo ambao utekelezaji wake umeanza Oktoba, 2014 na unategemewa kukamilika Juni, 2016 unatarajiwa kuhudumia wakazi 93, 267 sawa na asilimia 100 ya wakazi wote waishio Sengerema na vijiji jirani vinavyopitiwa na mradi huu.
Waziri
wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Inj. Gerson Lwenge akiwa na Mkuu wa Wilaya
wa Sengerema, Zainab Tulack (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka
ya Majisafi na Majitaka Mwanza (MWAUWASA), Inj. Anthony Sanga (kulia)
kwenye Tenki la Maji ambalo ni sehemu ya Mradi wa Majisafi na Usafi wa
Mazingira mjini Sengerema LV WATSAN II.
……………………………………………………………………………………………………..
Waziri wa Maji na Umwagiliaji,
Mhe. Inj. Gerson Lwenge amefanya ziara ya kikazi katika mikoa ya Mara na
Mwanza leo na jana katika harakati ya kutatua kero ya maji kwa
wananchi. Mhe. Lwenge ambaye ana dhamana ya kuinua na kuendeleza Sekta
ya Maji na Umwagiliaji, amekagua miradi mbalimbali katika maeneo tofauti
huku akizungumza na viongozi, wataalamu, wakandarasi na wananchi kwa
nia ya kutafuta suluhisho la kudumu la tatizo ya maji.
Lengo kubwa la ziara hiyo ni
kujua sababu ya kusuasua kwa utekelezaji wa baadhi ya miradi na kusukuma
utekelezaji wa miradi inayotekelezwa katika mikoa hiyo ikamilike kwa
wakati na kuleta matokeo mazuri kwa wananchi na maendeleo ya taifa kwa
ujumla. Katika ziara hiyo Mhe. Lwenge alitembelea miji ya Musoma, Magu, Mwanza na Sengerema.
No comments:
Post a Comment