MBUNGE
wa jimbo la Kilolo mkoani Iringa Mh. Venance Mwamoto amesema kuwa
lengo la wananchi wa Kilolo kumchagua kuwa mbunge wao ni kutaka
kuona analeta maendeleo jimboni na sio kuwavunjia heshima wapiga
kura wake kwa kuwa mbunge bingwa wa kusinzia bungeni ama kushiriki
vurugu zisizo na tija silengo la wana Kilolo .
Akizungumza leo katika
mkutano wake wa hadhara katika kata ya Ng’ang’ange mkutano wa
kuwashukuru wananchi wa Kilolo kwa kumchangua kuwa mbunge wao kwa
ajili ya kutaka kuona wilaya hiyo ya kilolo inapiga hatua katika
maendeleo na si vinginevyo .
Hivyo alisema kuwa mbali
ya kuwa wapo baadhi ya watu wachache hasa wapinzani wake katika
siasa ambao wanazunguka maeneo mbali mbali ya jimbo hilo na
kumchafua kuwa amefungiwa kwa muda wa miezi sita kushiriki vikao
vya bunge kwa madai ya kuuliza swali la kupigania maendeleo ya
Kilolo ,alitaka wananchi wa Kilolo kupuuza maneno hayo kwani hakuna
jambo kama hilo na yeye hajapata kufungiwa wala kuonyo bungeni .
“Naomba mtambue huu si
wakati wa kampeni ni wakati wa mimi kama mbunge wenu kwa
kushirikiana na rais Dr John Magufuli na madiwani kuona kazi ya
kuwaletea maendeleo wananchi inafanyika ila wapo wapinzani wachache
ambao wanazunguka katika minada na kueleza uzushi usio na kichwa wa
miguu kuwa eti mbunge wa Kilolo amefungiwa na Rais Dr Magufuli
kushiriki vikao vya bunge kwa madai kuwa kwanini nataka kujenga
chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali teule ya wilaya ya Kilolo
iliyopo Ilula”
Mbunge Mwamoto alisema maneno
hayo yasiwakatishe nguvu wananchi wa Kilolo kweani hakuna kitu kama
hicho na Rais hausiki na kumwajibisha mbunge wala diwani pia hata
sipika hajapata kumnyoshea kidole wala kumpa onyo lolote na kuwa
siku zote mti unaopigwa mawe ndio wenye matunda na yeye atazidi
kuwaletea maendeleo wananchi wake kama alivyoanza na kuwataka
wapinzani na wana CCM kuachana na siasa za majukwaani kwa sasa ni
muda wa kazi.
Hata hivyo mbunge
Mwamoto alisema kuwa lengo lake ni kufanya kazi kwa moyo wote ili
kuifanya wilaya ya kilolo isonge mbele zaidi kimaendeleo na katika
kuonyesha kwa vitendo kuwa yeye si mbunge wa kulala ni mbunge wa
kazi ataomba diwani wa kata hiyo kuandaa ukumbi wa kijiji ili alete
Runinga kwa ajili ya wananchi wakitoka shamba kufuatilia vikao vya
bunge ili kuona kama ni mbunge wa kusinzia bungeni ama kazi.
Alisema iwapo wananchi wake
watabahatika kuona anasinzia bungeni pindi atakaporejea kutoka
bungeni wasisite kumuuliza sababu ya yeye kusinzia bungeni. |
No comments:
Post a Comment