Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa
akisalimiana na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge baada ya
kuwasili kwenye kijiji cha Dutwa akiwa katika ziara ya mkoa wa Simiyu
Machi3, 2016.Kulia ni Mbunge wa Viti Maalum , Esther Midimu. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akitaka maelezo kutoka kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Simiyu, Onesmo
Lyanga kuhusu madai kuwa askari wa Usalama Barabarani mkoani humo
wanawatoza faini kubwa hadi sh 300,000/= waendesha bodaboda. Alikuwa
katika mkutano wa kuwaslimia wananchi kwenye kijiji cha Dutwa wilayani
Bariadi Machi 3, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kasim Majliwa
akikagua ujenzi wa nyumba ya kuishi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji
wa Bariadi akiwa akika ziara ya mkoa wa Simiyu Machi 3, 2016. (Picha na
Ofisi a Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kasim Majliwa
akikagua ujenzi wa nyumba ya kuishi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji
wa Bariadi akiwa akika ziara ya mkoa wa Simiyu Machi 3, 2016. (Picha na
Ofisi a Waziri Mkuu)
Wasanii wa Bariadi wapiga ngoma
wakati Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa alipowasili kwenye bwawa la
Ng’wansubuya wialayani Bariadi kufungua bwawa hilo Machi 3, 2016.(Picha
na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akifurahia baada ya kufungua bwawa la umwagiliaji la kijiji cha
Ng’wasubuya wilayani Bariadi akiwa katika ziara ya mkoa wa Simiyu Machi
3, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa
akikagua Bwawa la umwagiliaji la kijiji cha Ng’wasubuya wilayani
Bariadi akiwa katika ziara ya mkoa wa Simiyu Machi 3, 2016. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akiweka jiwe la msingi la Ofisi ya CCM ya wilaya ya Bariadi akiwa
katika ziara ya mkoa wa Simiyu Machi 3, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
…………………………………………………………………………………………..
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
ameiagiza Kamati ya Uchumi ya Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi ikutane
na wafanyabiashara wote ili wajadiliane na kupanga kiwango cha ushuru
kinachopaswa kutozwa kwenye mazao ya wilaya hiyo.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo
(Alhamisi, Machi 3, 2016) wakati akizungumza na mamia ya wananchi
waliofika kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa michezo
wa Dutwa, Wilayani Bariadi, mkoani Simiyu.
Amefikia uamuzi huo baada ya
kuona bango lililoshikwa na wananchi wakilalamikia kutozwa ushuru wa sh.
3,000/- kwa gunia moja la mazao badala ya sh. 1,000/- ya zamani.
“Masuala ya ushuru ni maamuzi
baina yenu na Halmashauri yenu lakini hiyo tozo imeongezwa sana kutoka
sh. 1,000/- hadi sh. 3,000/-. Ninaiagiza Kamati ya Ucumi ikae na
wafanyabiashara wote ili mjadili suala hili na mkubaliane kiwango cha
ushuru.”
“Wabunge pia waalikwe kwenye
kikao hicho na Mwenyekiti wa Halmashauri pamoja na Baraza la Madiwani
nalo pia lishiriki kikao hicho. Kama mnataka kupandisha ushuru ni lazima
mkubaliane viwango ili Watanzania wafanye biashara wakiwa na mapenzi na
nchi yao,” alisema huku akishangiliwa.
Hata hivyo Waziri Mkuu alifafanua
kwamba suala la kulipa ushuru ni la muhimu katika kuchangia makusanyo
ya kodi kwa ajili ya maendeleo ya nchi. “Ushuru ni lazima ulipwe lakini
pia ni lazima muwe mmekubaliana ni kiwango gani mnatoza. Makusanyo yote
haya tunayofuatilia kwa sasa ni matokeo ya watu kulipa kodi na ushuru
kama huu,” alisisitiza.
Wakati huo huo, Waziri Mkuu
amekataza tabia ya maafisa wa kutoza ushuru kudai fedha kabla mwananchi
hajauza mifugo wanapoileta mnadani kwani anakuwa amekuja kutafuta fedha.
Alikuwa akijibu hoja iliyotolewa
na mbunge wa viti maalum (CHADEMA), Bi. Gimbi Masabo ambaye alimweleza
Waziri Mkuu kwamba kuna tabia ya kutoza sh. 6,000/- kwa kichwa kwa kila
ng’ombe anayeswagwa kuingia eneo la mnada bila kujali kama mtu huyo
ameuza ng’ombe au hajauza.
“Hivi unawezaje kumtoza mtu
ushuru wakati hajauza chochote au wakati akiwa njiani kuelekea mnadani?
Ni bora umtoze mtu baada ya kuuza. Kumbukeni kuwa wananchi wetu wanakuja
mnadani ili wauze na kupata fedha ya kurudi nayo nyumbani, sasa nyie
mnamtoza kabla hajauza chochote au hata kama hajauza. Acheni hiyo
tabia,” alisema.
Alimtaka Mwenyekiti wa
Halmashauri hiyo, Bw. Robert Lweyo aimarishe usimamizi wa minada na
kujua idadi ya mifugo ambayo inaingizwa, inayouzwa na ile inayobaki
ambayo imeshindikana kuuzwa.
“Jipange wewe Mwenyekiti na timu
yako ya watoza ushuru mfuatilie agizo hili. Mkiwa wavivu ndiyo mnakuja
na maamuzi haya ya jumla jumla ya kuanza kutoza ushuru hata mtu akiwa
njiani anakuja mnadani kutafuta fedha,” alisema Waziri Mkuu.
Mapema, akitoa taarifa ya wilaya
hiyo, Mkuu wa wilaya ya Bariadi, Bw. Ponsiano Nyami alisema wilaya hiyo
inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa ofisi kwa sababu majengo ya
iliyokuwa ofisi ya wilaya hivi sasa yanatumiwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
hali iliyowalazimu wahamie kwenye ofisi za Halmashauri.
No comments:
Post a Comment