Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa Tengeru nje
kidogo ya Jiji la Arusha mara baada ya kuwasili kwa ajili ya Uzinduzi
rasmi wa Barabara ya Arusha-Holili/Taveta-Voi Km 234.3 uliofanyika
Tengeru nje kidogo ya jiji la Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Rais wa Kenya Uhuru
Kenyatta kabla ya uzinduzi rasmi wa Barabara ya Arusha-Holili/Taveta-Voi
Km 234.3 uliofanyika Tengeru nje kidogo ya jiji la Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais wa Kenya
Uhuru Kenyatta kabla ya uzinduzi rasmi wa Barabara ya
Arusha-Holili/Taveta-Voi Km 234.3 uliofanyika Tengeru nje kidogo ya jiji
la Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Rais wa Uganda Yoweri
Museveni kabla ya uzinduzi rasmi wa Barabara ya
Arusha-Holili/Taveta-Voi Km 234.3 uliofanyika Tengeru nje kidogo ya jiji
la Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama pamoja na Rais wa
Kenya Uhuru Kenyatta, Uganda, Yoweri Meseveni na Rais wa Zanzibar Ali
Mohamed Shein wakati Wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ukipigwa kabla
ya uzinduzi wa barabara ya Arusha-Holili/Taveta-Voi Km 234.3
uliofanyika Tengeru nje kidogo ya jiji la Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia ya wananchi wa Arusha
hawapo pichani kabla ya ya uzinduzi rasmi wa Barabara ya
Arusha-Holili/Taveta-Voi Km 234.3 uliofanyika Tengeru nje kidogo ya jiji
la Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katikati akiwaongoza Marais wa Kenya,
Uganda, Makamu wa Rais wa Sudani Kusini pamoja na Burundi kukata utepe
kuashiria uzinduzi rasmi wa mitambo itakayotumika katika ujenzi wa
barabara ya Arusha-Holili/Taveta-Voi Km 234.3 uliofanyika Tengeru nje
kidogo ya jiji la Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimwagilia mti maji pamoja na
Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(Nairobi) Gabriel Negata mara
baada ya uzinduzi wa barabara ya Arusha-Holili/Taveta-Voi Km 234.3
uliofanyika Tengeru nje kidogo ya jiji la Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Kenya Uhuru
Kenyatta mara baada ya sherehe za unzinduzi wa barabara ya
Arusha-Holili/Taveta-Voi Km 234.3 uliofanyika Tengeru nje kidogo ya jiji
la Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu
wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na viongozi mbalimbali wa
ndani na nje ya Nchi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali
Mohamed Shein mara baada ya sherehe za uzinduzi wa barabara hiyo
kukamilika.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mkurugenzi wa Benki ya
Maendeleo ya Afrika(Nairobi) Gabriel Negata mara baada ya uzinduzi wa
barabara hiyo ya Arusha-Holili/Taveta-Voi Km 234.3 uliofanyika Tengeru
nje kidogo ya jiji la Arusha. PICHA NA IKULU
…………………………………………………………………………………………………………….
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa
Uhuru Muigai Kenyatta, wameweka jiwe la msingi katika ujenzi wa
barabara ya Arusha – Holili – Taveta – Voi, yenye urefu wa kilometa
234.3 ambayo inaunganisha nchi za Tanzania na Kenya.
Hafla ya uwekaji wa jiwe hilo la
Msingi imefanyika katika eneo la Tengeru Mkoani Arusha na kuhudhuriwa na
viongozi wengine wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambao ni Rais wa
Jamhuri ya Uganda Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveni, Makamu wa pili wa
Rais wa Jamhuri ya Burundi Dkt. Joseph Butore, Mwakilishi wa Rais Paul
Kagame wa Jamhuri ya Rwanda ambaye ni Waziri wa Afrika Mashariki wa
Rwanda Mheshimiwa Valentine Rwabiza na Makamu wa Pili wa Rais Sudan
Kusini Mheshimiwa James Wan Iga.
Uzinduzi huo pia umehudhuria Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein.
Kwa upande wa Tanzania ujenzi wa
barabara hiyo unatakelezwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza
inahusisha ujenzi wa barabara ya njia nne kutoka Arusha hadi Tengeru
yenye urefu wa kilometa 14.1, na ujenzi wa barabara ya mzunguko yaani “Bypass”
yenye urefu wa kilometa 42.4. Awamu ya pili itahusisha ujenzi wa
barabara ya njia nne kuanzia Tengeru hadi Usa River yenye urefu wa
kilometa 8.2 na Kutoka Usa River hadi Holili mpakani mwa Kenya na
Tanzania yenye urefu wa kilometa 100.2
Gharama za upanuzi wa barabara ya
Arusha – Tengeru na barabara ya kuzunguka nje ya jiji la Arusha kwa
upande wa Tanzania ni shilingi bilioni 209.6, ambapo kati ya fedha hizo
Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) itatoa mkopo wa shilingi bilioni
190.2 na serikali ya Tanzania itatoa shilingi Bilioni 19.4.
Aidha Serikali ya Tanzania kwa
kushirikiana na Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ipo kwenye
mazungumzo na serikali ya Japan ili kupata mkopo wa ujenzi wa awamu ya
pili inayoanzia Tengeru hadi Holili.
Kwa upande wa Kenya, mradi huu
unahusisha ujenzi wa barabara mpya kwa sehemu ya Taveta hadi Mwatate
yenye urefu wa kilometa 100. Sehemu ya Mwatate hadi Voi ujenzi wake
umekamilika.
Akizungumza katika hafla hii,
Rais Dkt. John Pombe Magufuli ambaye ni mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki, amesema wananchi wa Afrika Mashari hawapaswi kuwa masikini na
kueleza kuwa mradi huo na mingine itakayotekelezwa chini ya ushirikiano
wa Jumuiya ya Afrika Mashariki itasaidia kuinua hali ya maisha ya
wananchi.
Kwa upande wao Marais Uhuru
Muigai Kenyatta wa Kenya, Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda na
wawakilishi wa marais wa Burundi, Rwanda, Sudani Kusini wameuelezea
mradi huo kuwa ni moja ya miradi muhimu ya kuimarisha uchumi wa jumuiya
ya Afrika Mashariki na wametoa wito kwa nchi zote wanachama wa jumuiya
hiyo kushirikiana kukuza biashara baina yake.
Viongozi hao wote wamekiri kuwa
Jumuiya hii yenye watu zaidi ya milioni 160, inayo nafasi ya kupiga
hatua kubwa za kiuchumi na kuondokana na umasikini, ikiwa italitumia
vizuri soko la pamoja kwa kubadilisha bidhaa kutoka nchi moja hadi
nyingine na kujenga viwanda vingi badala ya kuendelea kutegemea bidhaa
kutoka nje.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Arusha
03 Machi, 2016
No comments:
Post a Comment