Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili (MNH) akizungumza LEO katika mkutano kabla ya
uzinduzi wa chumba maalumu cha uangalizi wa wagonjwa wanaolazwa katika
chumba hicho (ICU) katika Jengo la Mwaisela. Kulia ni Naibu Waziri wa
Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamisi
Kigwangallah.
Rais wa Shirika lisilo la
Kiserikali la Gastrenterology Foundation kutoka nchini Ujerumani,
Profesa Meinhard Classen akizungumza LEO katika mkutano wa uzinduzi wa
chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU) kwenye Hospitali
ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
Naibu Waziri wa Afya na Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamisi Kigwangallah akizungumza
kwenye mkutano wa uzinduzi wa ICU katika hospitali hiyo Leo. Dk
Kigwangallah amemuagiza Kaimu Mkurugenzi wa hospitali hiyo kuongeza
vitanda kwa ajili ya wagonjwa wanaolazwa ICU na kufikia 100.
Naibu Waziri wa Afya na Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamisi Kigwangallah akikata utepe
LEO kwenye Jengo la Mwaisela-Muhimbili ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa
ICU hiyo.
Baadhi ya wauguzi na madaktari wakifuatilia mkutano huo leo
No comments:
Post a Comment