Rais Dkt John Pombe Joseph
Magufuli akisalimiana na Mbunge wa Arumeru Msshariki Mhe Joshua Nassari
aliyekuwa mmoja wa viongozi na wananchi waliojitokeza kwa wingi
kumpokea alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA)
tayari kuongoza Mkutano wa 17 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya
Afrika Mashariki utofanyika jijini Arusha.
Picha na IKULU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa
Mkoa wa Arusha Daudi Felix Ntibenda mara baada ya kuwasili katika Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa
Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki ,Kikanda na Kimataifa
Balozi Agustine Mahiga mara baada ya Kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia vikundi
mbalimbali vya ngoma za asili mara baada ya kuwasili katika uwanja wa
ndege wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia vikundi mbalimbali vya ngoma za asili mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wakazi wa
Arusha na Kilimanjaro waliofika Uwanja wa ndege wa KIA kumpokea.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha wageni
mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimatifa wa Kilimanjaro
(KIA). PICHA NA IKULU
………………………………………………………………………………………………………………….
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewasili Mkoani Arusha ambako pamoja
na mambo mengine ataongoza Mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi
wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika Jumatano tarehe
02 Machi, 2016 Mjini Arusha.
Katika uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) Rais Magufuli amelakiwa na viongozi
mbalimbali wa vyama vya siasa na serikali pamoja na vikundi vya burudani
za ngoma kabla ya kuelekea Arusha Mjini.
Rais Magufuli ndiye Mwenyekiti wa
sasa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki inayojumuisha nchi za Tanzania,
Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.
Kabla ya kuongoza kikao hicho
Rais Magufuli anatarajiwa kukutana na kufanya mazungumzo ya ana kwa ana
na viongozi wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Tarehe 03 Machi, 2016 Rais
Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Kenya, wataweka jiwe la msingi katika
mradi wa ujenzi wa barabara ya Arusha – Holili – Taveta – Voi
inayoziunganisha nchi za Tanzania na Kenya.
Barabara hiyo ni sehemu ya miradi ya maendeleo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki inayotekelezwa na nchi wanachama wa Jumuiya hiyo.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.
Dar es salaam
02 Machi 2016
No comments:
Post a Comment