MWENYEKITI WA SHIRIKA LA SHIKUJANJO AKISOMA TAARIFA MBELE YA MGENI RASMI
MWENYEKITI WA BODI YA SHULE YA SEKONDARI MABATINI ANDREW MTEGA AKITOA NASAHA KWA WANAFUNZI
MGENI RASMI AFISA UTAMADUNI NA MICHEZO MKOA WA NJOMBE STIVEN SANGA AKITOA HOTUBA YAKE
HAWA NI WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI MABATINI WAKIWA KWENYE MKUTANO HUO
HUU NI MSAADA ULIOTOLEWA NA SHIRIKA LA SHIKUJANJO KUPITIA WAFADHILI
MKUU WA SHULE YA SEKONDARI MABATINI NJOMBE GENOVEVA KIKUDO AKIWAONESHA VILIKO HIFADHIWA VIFAA VYA MAABARA
Katibu Tawala Mkoa Wa Njombe Jackson Saitabahu Amepongeza Shirika La Kujenga Uwezo Kwa Jamii Mkoa Wa Njombe SHIKUJANJO Kupitia Ufadhili Wa Ubalozi Wa Marekani Kwa Kutoa Msaada Wa Vifaa Vya Masomo Ya Sayanzi Katika Shule Ya Sekondari Mabatini Vyenye Thamani Ya Zaidi Ya Shilingi Milioni 12 Vilivyotolewa Kwa Vipindi Viwili.
Akizungumza Wakati Wa Kukabidhi Msaada Huo Akiwa Mgeni Rasmi Kwa Niaba Ya Katibu Tawala Mkoa Wa Njome Jackson Saitabahu,Afisa Utamaduni Na Michezo Mkoa Stiven Sanga Ametaka Wanafunzi Kutumia Fursa Hiyo Kuyapenda Masomo Ya Sayansi Na Kuondoa Dhana Ya Kwamba Masomo Hayo Ni Magumu Kuliko Mengine.
Aidha Bwana Sanga Amesema Changamoto Ya Kukosekana Kwa Vifaa Vya Masomo Ya Sayansi Katika Shule Ya Sekondari Mabatini Imetatuliwa Kupitia Ushirikiano Wa Walimu Na Shirika La Shikujanjo Ambapo Ametaka Walimu Na Wanafunzi Kutunza Kwa Umakini Vifaa Hivyo Ili Viweze Kudumu Na Kuwanufaisha Vizazi Na Vizazi Vijavyo.
Mwenyekiti Wa Bodi Ya Shule Ya Sekondari Mabatini Andrew Mtega Ametaka Wanafunzi Wa Shule Hiyo Kuonesha Ushirikiano Katika Kuwabaini Waharifu Ambao Wanahusika Na Wizi Wa Vifaa Vya Shule Ili Hatua Kali Zichukuliwe Dhidi Yao Hata Kama Ni Mwalimu Ama Mwanafunzi Na Kujenga Uaminifu Kwa Wafadhili Huku Akishukuru Kwa Msaada Huo.
Akizungumza Mara Baada Ya Kukabidhiwa Msaada Huo Mkuu Wa Shule Ya Sekondari Mabatini Genoveva Kikudo Amesema Msaada Huo Utawasaidia Wanafunzi Wa Shule Hiyo Kufanya Vizuri Katika Masomo Ya Sayansi Na Kuinua Kiwango Cha Taaluma Huku Akisema Shule Hiyo Inamikakati Ya Kuongeza Ufaulu Wa Masomo Ya Sayansi.
Kwa Upande Wake Mwenyekiti Wa Shirika La Kujenga Uwezo Kwa Jamii Mkoa Wa Njombe Lameck Kinyunyu Amesema Msaada Uliotolewa Kwa Siku Ya Jana Una Gharimu Zaidi Ya Shilingi Milioni Mbili Ambapo Fedha Hiyo Inafanya Zaidi Ya Shilingi Milioni 12 Za Vifaa ViliVYotolewa Kipindi Kilicho Pita Ambazo Shirika Hilo Limepata Kwa Wafadhili Wa Marekjani.
No comments:
Post a Comment