Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Paul Makonda akizungumza na waandishi wa
habari leo jijini Dar es salaam leo wakati alipozungumzia mpango wa
kuwasafirishwa walimu bure jijini Dar es salaam wakati wa kwenda na
kurudi kazini huku akiwa ameongozana na viongozi wa vyama vya
usafirishaji wa abiria jijini Dar es salaam pamoja na viongozi wa
Madereva wa Daladala jijini Dar es salaam.(Picha na Geofrey Adroph wa
Pamoja Blog)
Mwenyekiti
wa Chama Chama Wamiliki wa Daladala Mkoa wa Dar es salaam, Said
Mabrouk(wa kwanza kushoto) akizungumzia mwitikio wa wamiliki hao kuhusu
kuwasafirisha walimu ili kuunga mkono juhudi za Mkuu wa Wilaya ya
Konondoni Mh. Paul makonda na Rais Dk. John Pombe Magufuli katika kutoa
elimu bure hapa nchini, kutoka kulia ni Makamu mwenyekiti wa Umoja wa
Madereva, Shabani Mdemu, wa pili kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Umoja wa
Wasafirishaji abiria Dar es Salaam, (UWADAR),William Masanja.
Mwenyekiti
wa Umoja wa Wasafirishaji abiria Dar es Salaam, (UWADAR),William
Masanja akizungumza na waandishi wa habari leo jijinni Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kazini
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
WALIMU wa Shule ya Msingi na Sekondari Mkoa wa Dar es Salaam watasafiri na Daladala bure kuanzia Machi 7 mwaka huu.
Akizungumza
na waadishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Wilaya ya
Kinondoni, Paul Makonda amesema kuwa kutokana na changamoto za walimu
ameona kuna umuhimu wao kusafiri bure waweze kupunguza makali ya nauli
za kila siku wanapopanda daladala hizo.
Amesema
kuwa walimu watasafiri kwa usafiri huo kuanzia saa 11:30 hadi saa 2
kwa muda wa asubuhi na baada ya muda huo kupita watalipa nauli zao na
nyakati za jioni watarudi majumbani mwao kwa kupanda daladala hizo
kuanzia saa 9 hadi saa 12.Makonda
amesema kuanzia kesho watatengeneza vitambulisho vya walimu wote wa
serikali wa mkoa wa Dar es Salaam ambavyo wataonyesha kwa makondakta wa
daladala vikiwa na saini ya mkuu mkuu wa Wilaya.
Amesema
utaratibu huo utakuwa ukitumika kwa siku za kazi tu kwa walimu kupanda
bure na sio vinginevyo na walimu wanaoishi mikoa mingine na wanafundisha
Dar es Salaam watalipa nauli zao kufika katika vituo vyao vya kazi.
Aidha
amesema kuwa walimu wataingia katika Daladala wasiopungua wawili na
wengine watasubiri daladala zingingine kutokana na maoni ya wamliki wa
vyombo vya usafiri.Nae Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa Daladala Mkoa
wa Dar es Salaam, Sabri Mabroock amesema kuwa wanaunga mkono sera ya
elimu ya Rais Dk.John Pombe Magufuli.
Amesema
walimu wamekuwa na changamoto wakati mwingine wanashindwa kulipa hata
nauli hivyo kupanda bure watakuwa wamerahisisha maisha.
No comments:
Post a Comment