Eneo
la vijiji vya Pawaga linavyoonekana kwa picha za angani wakati wa Naibu
Waziri, Dk. Kigwangalla alipo dhuru kwa kutumia Chopa.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.
Hamisi Kigwangallla amekuwa kiongozi wa kwanza wa ngazi za juu kufika
katika eneo lililokumbwa na mafuriko katika vijiji vya Mbolimboli,
Tarafa ya Pawaga iliyopo Iringa vijijini Mkoani hapa ambapo mbali na
kutoa pole pia ameweza kutoa huduma za kitabibu kwa baadhi ya watu
waliozidiwa waliokuwa bado hawajaokolewa.
Awali
Dk. Kigwangalla alipodhuru kwa wananchi waliopo kwenye kambi ya muda
baada ya kunusurika na mafuriko hayo, aliwaeleza kuwa Serikali
itaendelea kushirikiana nao bega kwa bega kwani Serikali ya “Hapa Kazi
Tu” haina ngoja ngoja ndio maana yeye ameweza kufika haraka kuakikisha
wananchi wapo salama na wanapatiwa huduma zote za msingi na za kijamii
ikiwemo matibabu na elimu ya kijikinga na milipuko ya magonjwa ikiwemo
magonjwa ya kipindupindu ambacho kimewakumba wananchi hao.
Dk.
Kigwangalla ameweza kufanya hilo baada ya Chopa iliyokuwa ikimtembeza
angani kufika katika maeneo yaliyozingirwa, alimuru rubani wake kushusha
chini na kisha kutoa msaada wa haraka kwa akina mama na watoto
waliokuwa wamezingirwa kwenye moja ya maeneo hayo zaidi ya siku tatu
bila kuokolewa ambapo alitoa huduma na kisha Chopa hiyo iliwabeba hadi
katika eneo maalum waliopo wahanga wengine waliookolewa.
Pia
Dk. Kigwangalla aliweza kutoa elimu na maelekezo mbalimbali kwa wahanga
hao kujiepusha na masuala ya kutumia mahitaji salama ilikuepukak
kipindupindu kisienee zaidi kwani hadi sasa eneo hilo limeweza
kupatikana wagonjwa wa ugonjwa huo zaidi ya 220 huku hadi wanatembelea
katika kambi ya Mtakatifu Lucas iliyopo Pawaga, ilikuwa na wagonjwa
zaidi ya 40.
Imeandaliwa na Magreth Kinabo–MAELEZO, Andrew Chale, modewjiblog-Iringa
Naibu Waziri, Dk. Kigwangalla alipo dhuru kwa kutumia Chopa katika eneo lililokumbwa na mafuriko hayo kijiji cha Mbolimboli
Baadhi ya wananchi waliookolewa baada ya Naibu Waziri, Dk.Kigwangalla kuamuru wawaishwe katika kambi waliopo wahanga wengine.
Naibu
Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla akipewa maelezo namna wanawake hao
pamoja na watoto wao wadogo walivyoweza kuzingirwa na maji kwa muda wa
siku tatu bila kuwa na huduma muhimu ambapo hata hivyo, Naibu Waziri
aliweza kuwasaidia ikiwemoo kuamuru Chopa hiyo iwapeleke kwenye kambi
maalum na kisha wao kubaki hapo kabla ya kurudiwa tena na kuendelea na
safari ya Kambi ya watu wa Kipihdupindu.
Naibu
Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla akipata maelezo ya mmoja wa waokoaji
wanaotumia boti maalum namna walivyoweza kupata taabu jinsi ya uokoaji
katika eneo hilo.
Baadhi
ya wahanga wa mafuriko wa vijiji vya Mbolimboli katika Tarafa ya Pawaga
wakipata maji maalum yenye dawa ilikujikinga na ugonjwa wa kipindupindu
ambao hata hivyo umeenea katika eneo hilo kutokana na maji yake
kuchafuliwa na vinyesi vya vyoo vilivyokumbwa na mafuriko.
Naibu
Waziri, Dk.Kigwangalla akisisitiza wahanga hao wa mafuriko kuakikisha
wanatumia vyakula na vitu vingine kwa hali ya usafi ilikueupuka ugonjwa
huo wa kipindupindu.
Baadhi
ya akina mama wakipanda Chopa baada ya Naibu Waziri wa Afya, Dk.
Kigwangalla kuamuru wapelekwe kwenye kambi haraka kutokana na watoto
waliokuwa nao kuzidiwa (wanawake hao wanaoonekana pichani ndani ya
chopa).
Naibu
Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Iringa
wakiwa katika Chopa juu wakiangalia namna mafuriko hayo yalivyosababisha
athari kubwa na kufanya kuwa kisiwa katika vijiji hivyo vya Mbolimboli.
eneo la chini linavyookena kutokana na mafuriko hayo.
Naibu
Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla akioneshwa moja ya maeneo namna maji
yake yalivyochafuliwa na kinyesi baada ya vyoo kuharibiwa na mafuriko
hayo.
Baadhi
ya wananchi wakimsikiliza Naibu Waziri, Dk. Kigwangalla (hayupo
pichani) wakati alipofika katika eneo lililokuwa akina mama hao na
watoto ambao wamekaa siku tatu bila kupata huduma muhimu.
Pichani
ni baadhi ya akina mama na watoto ambao walikwama kwa zaidi ya si tatu
kwenye mafuriko hayo huku wakishindwa kupata mahitaji muhimu ambapo pia
vifaa vya uokoaji na waokoaji kushindwa kuwafikia ambapo hata hivyo
Naibu Waziri wa Afya. Dk. Kigwangalla alipoamuru Chopa iliyokuwa ikipita
kuangalia athari hizo kushuka kisha kuwachunguza na kupelekwa kwenye
kambi maalum.
uokoaji ukiendelea..
Naibu
Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Iringa,
wakielekea katika kambi ya wahanga hao wa mafurikoeneo la Itunundu..
No comments:
Post a Comment