Kamishna Jenerali John Casmir
Minja akipokea Salaam ya Utii kutoka kwa Gadi Maalam iliyoandaliwa na
Maofisa wa Jeshi la Magereza, Wahitimu wa Mafunzo ya Udereva(hawapo
pichani) katika Chuo cha Udereva Kingolwira Mkoani Morogoro. Hafla hiyo
imefanyika katika Viwanja vya Chuo hicho 16 Februari, 2016.
Kamishna Jenerali wa Magereza
John Casmir Minja akikagua Gadi Maalum iliyoandaliwa na Wahitimu wa
Mafunzo ya Udereva katika Chuo cha Uderevau na Ufundi Kingolwira, Mkoani
Morogoro.
Wahitimu wa Mafunzo hayo wakipita mbele ya Mgeni rasmi katika mwendo wa kasi kama wanavyoonekana katika picha.
Kamishna Jenerali wa Magereza
John Casmir Minja akipokea taarifa fupi Ofsini kwa Mkuu wa Chuo cha
Udereva na Ufundi Kingolwira, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Osmond
Nduguru(hayupo pichani).
Kamishna Jenerali wa Magereza,
John Casmir Minja akimtunuku cheti Askari Mhitimu wa Mafunzo ya Udereva
kwa niaba ya Wahitimu wote wa mafunzo hayo.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wa
Mkoani Morogoro wakifanya Mahojiano Maalum na Kamishna Jenerali wa Jeshi
la Magereza, John Casmir Minja.
Mgeni rasmi, Kamishna Jenerali wa
Magereza John Casmir Minja(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na
Wahitimu wa Mafunzo ya Udereva katika Chuo cha Udereva na Ufundi,
Kingolwira Mkoani Morogoro.
…………………………………………………………………………………………….
…………………………………………………………………………………………….
Na Lucas Mboje; Morogoro
MADEREVA wote wa magari ya Jeshi
la Magereza nchini wametakiwa kuzingatia Sheria za Usalama Barabarani
wakati wote wanapoendesha magari ili kujiepusha na ajali zisizo za
lazima.
Rai hiyo imetolewa na Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini, John Casmir Minja wakati akizungumza kwenye
hafla ya kufunga Mafunzo ya Udereva Kozi ya Msasa kwa Maofisa wa Jeshi
la Magereza kutoka Mikoa yote Tanzania Bara yaliyofanyika katika Chuo
cha Udereva na Ufundi, Kingolwira Mkoani Morogoro.
Jenerali Minja amewaagiza
Wahitimu wa Mafunzo hayo kuhakikisha kuwa wanawajibika pia kuyatunza
magari watakayokabidhiwa kuyaendesha ili yaweze kudumu kwa muda mrefu
kama ilivyokusudiwa.
“Nawataka mjiepushe na uzembe
wakati mnapoendesha magari ya Jeshi letu ikiwa ni pamoja na
kutokujihusisha na ulevi na kuendesha magari hayo kwa mwendo kasi bila
kuzingatia Sheria za Usalama Barabarani”. Alisema Jenerali Minja.
Aidha Jenerali Minja amezungumzia
upungufu mkubwa wa magari katika Jeshi hilo ambapo katika
kushughulikia changamoto hiyo Jeshi la Magereza kupitia Wizara ya Ulinzi
na Jeshi la Kujenga Taifa limesaini Mkataba na Kampuni za Ashok Layland
na Jeep na magari mia tisa na tano(905) yanategemewa kupokelewa mapema
mwanzoni mwa mwezi Mei Mwaka huu.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha
Udereva na Ufundi Kingolwira, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Osmond
Ndunguru kupitia risala yake kwa Mgeni rasmi amesema kuwa Wahitimu hao
wamejifunza Mafunzo yote yaliyopo kwenye Mtaala wa Mafunzo ya Udereva
kwa nadharia na vitendo ikiwemo mbinu mbalimbali katika fani ya Udereva
wa Magari ambapo jumla ya Wanafunzi 125 wamehitimu Mafunzo hayo miongoni
mwao Wanaume ni 133 na wa kike ni 2.
Aidha Kamishna Msaidizi wa
Magereza, Nduguru alieleza changamoto mbalimbali ambazo Chuo hicho
kinakabiliana nazo ikiwemo upungufu wa magari ya kujifunzia pamoja na
uchakavu wa miundombinu ya majengo hali inayoathili utoaji taaluma ya
mafunzo hayo.
Chuo cha Udereva na Ufundi cha
Kingolwira, kilichopo Mkoani Morogoro kinamilikiwa na Jeshi la Magereza
ambacho hutoa Mafunzo ya Udereva kwa Maofisa wa Jeshi la Magereza ambao
huendesha magari ya Jeshi hilo na katika Taasisi mbalimbali za Umma
hapa nchini.
No comments:
Post a Comment