WaziriwaElimu,
Sayansi, Teknolojia na Ufundi Prof.Joyce Ndalichako akifafanua jambo
mbele ya waandishi wa habari kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo
Tarishi Maimuna Kibenga. Picha na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Na CHalila Kibuda, Globu ya Jamii.
Waziri
wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako,
ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mteandaji wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya
Juu (HELSB), George Nyatage kutokana na kuwepo na ukiukaji wa utoaji wa
mikopo pamoja na ucheleweshaji usio kuwa na sababu za msingi.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Profesa Ndalichako
amesema kuwa bodi ya mikopo imekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa
wanafunzi wanaostahili kupata mikopo ya kufanya kwao kuweza kupata
mikopo mpaka waandamane wizarani kwa kusababishwa na watu wa wachache wa
bodi hiyo.
Kutokana
na udhaifu wa kiutendaji wa bodi hiyo baada ya kutengua uteuzi wa
Mkurugenzi Mtendaji, watendaji watatu wa bodi hiyo wamesimamishwa kazi
ambao ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Yusufu Kisare, Mkurugenzi wa
Urejeshaji wa Mikopo, Juma Chagonja pamoja na Mkurugenzi wa Upangaji na
Utoaji Mikopo, Onesmo Laizer.
Profesa
Ndalichako, amesema katika udhaifu wa utendaji huo ni pamoja ni ulipaji
wa mikopo kwa wanafunzi 23 walilipwa katika vyuo viwili tofauti kwa
miaka mitatu mfululizo kwa chuo cha kwanza zililipwa zaidi ya sh.milioni
653 na chuo cha pili ni zaidi ya sh. milioni 147.
Amesema
baadhi ya wanafunzi ambao walikwenda kusoma nchini Algeria wamekuwa
wakiendelea kulipwa fedha wakati mkataba wao umekwisha kwa kipindi cha
miaka saba.
Profesa
Ndalichako amesema wanafunzi 169 walipata mikopo katika vyuo viwili
tofauti kwa miaka mitatu mfululizo na kulipa chuo cha kwanza zaidi ya
sh.milioni 658 na chuo cha pili zaidi ya sh. milioni 665 na wanafunzi 55
walioacha masomo walilipwa zaidi ya sh.milioni 136 huku wanafunzi 343
wasiokuwa na usajili kwenye vyuo husika walilipwa zaidi ya sh.milioni
342.
Aliongeza
kuwa zaidi ya sh.milioni 159 zililipwa kwa wanafunzi 306 zaidi ya
kiwango kilichobainishwa kutokana na muongozo wa upangaji na ukopeshaji
wa mwaka 2008/2009 na 2009/2010.
Aidha
amesema kuwa wanafunzi 77 walipatiwa mikopo kwenye vyuo vya ndani na
nje ya nchi kwa wakati mmoja ambapo walilipwa zaidi ya sh.milioni 467
kwa vyuo nje na zaidi ya sh.milioni 123 kwa vyuo ndani pamoja na
wanafunzi 19,348 walipata mikopo bila kupitiwa na kamati ya mikopo jambo
ambalo ni kinyume na kanuni na 8ya kanuni za mikopo ya wanafunzi wa
elimu ya juu.
Hata
hivyo amesema wanafunzi 54,299 walipangiwa mikopo wakati hawakuwa
wameomba ambapo walilipwa zaidi y ash.milioni 207 ambazo zilipelekwa
kwenye vyuo sita.
No comments:
Post a Comment